Jarida La Cheche Za Fikra Toleo Na. 22

  • Uploaded by: Subi
  • 0
  • 0
  • December 2019
  • PDF

This document was uploaded by user and they confirmed that they have the permission to share it. If you are author or own the copyright of this book, please report to us by using this DMCA report form. Report DMCA


Overview

Download & View Jarida La Cheche Za Fikra Toleo Na. 22 as PDF for free.

More details

  • Words: 2,233
  • Pages: 4
M O T O WA MA BA DI L I K O UM E ANZ A . . .

Cheche za Fikra

J U ZU U 6 TO LE O 22 J AN U A RI 1 3 , 2 0 09

KIJARIDA CHA BURE— UKISHASOMA MPE MWINGINE—USIBANIE!

UCHAGUZI WA UWCCM

WAZIRI SIMBA ASEMA HAKUPENDELEWA kuliko vile vya wagombea wengine.

Mwenyekiti mpya wa UWCCM(T) Mhe. Sofia Simba

Na. Fred Katunzi Mwenyekiti mpya wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWCCM) Mhe. Sophia Simba (CCMKuteuliwa) amesema kwamba uchaguzi wake

Akizungumza na mwandishi wetu siku ya Jumapili Mhe. Simba ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) amesema kwamba kuingia kwake kwenye mchakato wa uchaguzi huo kwanza kabisa ilikuwa ni katika kupima jopo la wagombea nafasi hiyo ili kuona nani atafaa na yule ambaye atakuwa ana vigezo vinavyostahili basi ndiye atapaswa kuiongozi jumuiya hiyo ya Chama cha Mapinduzi.

kwenye nafasi hiyo Vyombo vya habari mwishoni mwa juma “Mimi haukutokana na nilichukua havikutupima mbele ya kubebwa na kiongozi fomu yeyote au kucheza rafu wananchi! nikiamini bali kutokana na ya vigezo vya kiuongozi kwamba alivyonavyo ambavyo vilikuendapo atatokea mtu mwingine balika zaidi na wapiga kura mwenye uwezo zaidi na anayefaa

Benjamin. G. Mwalukasa

Kijarida Ulichoshika • Kinatoka kila Jumanne • Ni cha bure kabisa! • Kisichofungamana na chama chochote au fisadi yeyote! • Kiko huru, kinathubutu, na hakiogopi mtu au hoja yoyote. • Ni kijarida chako! • Haki zote za kuchapa na kunakili zimeruhusiwa!

Ndani ya Toleo Hili

HOJA YA MWANAKIJIJI — CHADEMA WAMEZEMBEA MBEYA—2

Ushindi wa Sofia Simba

(Inaendelea toka toleo lililopita) KUBALIKA KITAIFA. Mpaka pale watakapojiweka kwenye Leo hii, nina imani kuwa waki- nafasi hiyo ndipo tunaweza fanya mabadiliko ya hapa na kuzungumzia dhamana ya kupale upinzani unaweza kujiliongoza Taifa. Sasa hivi kwa weka katika nafasi ya kukumiaka karibu hamsini hii, ni balika kitaifa. Narudia tena kauli CCM ndiyo imeweza kushika hii ili izame: WAKIFANYA MAhatamu za uongozi wa Taifa. BADILIKO YA HAPA NA PALE UPINZANI UNAWEZA KUJISasa kutakuwa hakuna mvuto WEKA KATIKA NAFASI YA KU- tena huko Mbeya Vijijini

Chadema na CUF

1

Chadema na CUF

2

Kuhusu Mapinduzi

3

Jessica: Zali la mafuta

3

Maoni ya Mtandao

4

Picha na Katuni

4

maana wengine tulikuwa tunasubiri hiyo “showdown” kati ya CCM na Chadema, unaonaje? Kuangalia nchi kama vyama viwili tu ni makosa. Naamini hii ni nafasi kwa chama cha CUF kuonesha kuwa kinaweza kushinda tena Tanzania bara na tena kwenye (inaendeleaUk.2)

1, 2

PAGE 2

CHECHE ZA FIKRA

SIJAPENDELEWA—SOFIA SIMBA zaidi basi mimi nisingirerudisha fomu” alisema Mhe. Simba akielezea sababu ya yeye kuamua kugombea nafasi hiyo. “Mwishoni nikaona kuwa waliochukua walikuwa ni wagombea dhaifu zaidi na hivyo nikaamua kuendelea na kujaribu kwangu kugombea nafasi hiyo” alisema. Alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kuwa na vigezo zaidi vya uongozi Mhe. Simba alikiri kwamba mojawapo ya upungufu kuelekea uchaguzi huo ni vyombo vya habari kutoandika kuhusu sifa za wagombea ili kutoa mwanga zaidi kwa wapiga kura kuweza kuamua ni nani anafaa. “vyombo vingi vya habari havikutupima mbele ya wananchi, vingi vilikuwa vinaandika zaidi kuhusu mambo hata yasiyo na msingi”Alidai Mhe. Simba. “Ninaamini mimi nilikuwa mgombea bora zaidi kwa kipimo chochote kile. Kielimu nina shahada mbili moja ya kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (Sheria) na pia kutoka New Hampshire, Marekani kwenye mambo ya (Maendeleo ya Kiuchumi ya Kijamii). Alipoulizwa kuhusu kigezo hicho cha elimu kuwa ndiyo msingi wa wagombea kuchujwa na yawezekana kiongozi mzuri anaweza hata asiwe mwenye

elimu Mhe. Simba alisema kuwa “katika karne hii ya 21 suala la elimu haliwezi kuwekwa pembeni, kwani mwenye elimu ana mchango wa pekee kuliko mtu ambaye hana elimu”. Akizungumza na mwandishi wetu kwa kirefu kuhusu suala hilo na hasa hisia za baadhi ya watu kuwa yawezekana kutokana na maneno ya Rais wakati wa kufungua mkutano huo kuwa wajumbe wachague watu wasomi yalikuwa ni kama kumpigia yeye debe Mhe. Simba alionesha Magazeti haya kushangazwa na watu wenye mawazo ya namna hiyo. “Unategemea Rais aseme yanahaririwa na watu wachague mtu asiye na elimu? Rais wahariri wale wale alisema kitu ambacho ni cha msingi kuwa uongozi katika chama sasa uendane na elimu pia” alifafanua. Alipohojiwa kwanini yeye ambaye tayari ni Mbunge na ana wajibu mkubwa wa Uwaziri agombee nafasi nyingine katika chama Mhe. Simba alisema kuwa “hii ni nafasi katika chama changu na hilo siyo jambo geni kwani hata mwenyekiti aliyetangulia (Mhe. Anna Abdallah) amekuwa Mwenyekiti kwa muda mrefu na pia amewahi kushika nafasi za Uwaziri vile vile, kwa hiyo siyo jambo geni”. Pamoja na hayo Mhe. Simba aliongeza kuwa “Kuna faida pia ya kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya na Waziri vile vile, kwani serikali iliyoko madarakani ni serikali ya CCM

hivyo mambo ambayo yanaibuliwa na kina mama wa UWCCM yanapata sauti pia katika serikali moja kwa moja”. Alipoulizwa kuhusu maneno mengi yaliyokuwa yamesambaa wakati wa kampeni hasa kati yake na mpinzani wake mkubwa Mhe. Janeti Kahama, Mhe. Simba alisema kuwa “yote hiyo ilikuwa ni kampeni” na ya kuwa hana kinyongo na mtu yeyote na huu ni wakati wa kuleta mabadiliko katika UWCCM ili iwe jumuiya yenye nguvu zaidi na inayowavutia wanawake wote. “UWCCM ina mtandao mkubwa kuanzia kijijini hadi Taifani, hivyo ofisi hizi zinaweza kabisa kuwa chachu ya maendeleo katika jamii. Hivyo tutaifanya jumuiya kuwa ni chombo cha wanawake na ninaamini kuwa chama changu kitafanya jumuiya hii kuwa ni mkombozi wa wanawake” alisema Mhe. Simba. Aliahidi kuwa kutokana na uzoefu wake wa nafasi mbalimbali ikiwemo ya Uwaziri wa Jinsia, Watoto na Maendeleo ya Jamii “niko tayari kuleta mabadiliko katika UWCCM ili kumfanya mwanamke aweze kushirikiana na wengine na pia kuweza kutumia fursa mbalimbali kujiletea maendeleo.” Mahojiano hayo yatasikia Jumatano kwenye mwanakijiji.com (M– Podcast)

HOJA YA MWANAKIJIJI: CHADEMA IUNGE MKONO CUF

Maalim Seif Sharrif Hamad (CUF) eneo ambalo si la kawaida “kwake”. CUF ina raslimali zaidi kuliko chama kingine chochote cha upinzani nchini lakini kwa muda mrefu hakijazama sana Tanzania bara na nafasi hii ni nafasi yao kuonesha wanakubalika na wanaweza. Ni kwa sababu hiyo naamini itakuwa

vizuri vyama vingine vya upinzani (ikiwemo Chadema) vikiiunga mkono CUF ili kushinda. Hata kama si kwa sababu ya kukikubali au kukubaliana nacho bali kwa kanuni ya kutaka kukataa kuipa CCM njia nyeupe. Kuna msemo kuwa “adui wa adui yangu, ni rafiki yangu”. Hivyo, kuna matatizo kati ya CUF na Chadema wakati huu wanatakiwa kuyaweka matatizo yao pembeni na kuunganisha nguvu na wakitaka kuyaendeleza watayaendelea baadaye. Unafikiri hilo litafanyika? Inategemea vichwa vilivyopo. Kama kuna vichwa vyenye kisasi, hasira, na kinyongo basi sitarajii kuona hilo likifanyika. Inahitaji uongozi madhubuti, muono wa mbali, ujasiri wa kuthubutu na kuweka kanuni mbele kuliko furaha

ya muda. Sioni ni nani ndani ya Chadema anayeweza kusimamia kanuni hiyo. Tusubiri tuone. Kwanini inaonekana kama unapigia debe upinzani, unataka CCM ishindwe? Kwangu mimi kushindwa kwa CCM ni suala la kanuni. CCM bado haijalipishwa gharama ya vitendo vya ufisadi nchini. Gharama ya utawala wa kibabe, wala gharama ya utawala wa kubebana. Kama chama CCM hakijaadhibiwa kwa yale yaliyotokea chini ya utawala wake. Na adhabu ya kweli inatokea kwenye sanduku la kura. Kwa wengine wanafikiri Tarime iliwauma sana CCM, hapana haikuuma sana kwani halikuwa jimbo lao. Kitakachokuwa kimewauma labda ni sifa zao tu na kiburi chao lakini zaidi ya hapo hakuna. Ndiyo maana nilishangazwa na watu (inaendelea Uk. 3)

KARIBU MWANAKIJIJI.COM

JUZUU 6, TOLEO 21 CCM itamtema mzee Makamba kwa kuanguka Tarime. Lakini kama wakianguka Mbeya Vijijini hapo kitawauma kwani watakuwa wamepoteza jimbo “lao”. Hivyo kwangu kushindwa kwa CCM kwenye uchaguzi wowote ni kwa sababu ningependa kuona CCM inaumizwa na kuguswa na kuoneshwa kuwa isipobadilika itaendelea kupoteza kura na hatimaye uongozi wan chi. Hadi hivi sasa CCM haijaonja machungu ya kupoteza viti vya ubunge kwenye uchaguzi mdogo. Ndiyo maana majimbo yanayouma sana ni yale ambayo CCM iliamini inakubalika na kuyapoteza (Moshi Mjini kwa mfano). Hata hivyo ukiangalia majimbo hayo makosa yalikuwa ya CCM wenyewe CCM ikionja kushindwa, ndipo itafanya hima kubadilika; kwa kadiri inazidi kuzawadiwa ushindi inazidi kuwa na ile hisia ya uhodhi wa utawala wa nchi. Hivyo kwangu kutaka CCM ishindwe siyo sababu ya chuki bali kanuni ya kuwajibishwa ifanye kazi.

PAGE 3

HOJA YA NGUVU HISTORIA YA MAPINDUZI IANDIKWE KWA UWAZI Na. Ben Mwalukasa Kuna matukio katika Muungano wetu ambayo yanapaswa kupitiwa tena kwa upya na historia yake kuandikwa kwa uhuru na uwazi ili kuwa hazina kwa vizazi vijavyo. Kuna matukio kama ya harakati za uhuru, uasi wa jeshi mwaka 1964, kutangazwa Azimio la Arusha mwaka 1967, vijiji vya ujamaa n.k Hata hivyo kati ya hayo yote naamini Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 yanabakia kuwa yenye utata wa kihistoria kuliko matukio mengine ya kisiasa nchini. Bila ya shaka wanasiasa wetu watakuwa wameyasifia Mapinduzi hayo jana katika kilele cha sherehe za Mapinduzi. Hata hivyo, naamini baadhi ya matatizo, mgongano na mgawanyiko tunaouona

Zanzibar leo hii umetiwa alama ya kudumu katika mapinduzi hayo. Kwa muda mrefu kumekuwa na majaribio ya kutotaka kabisa kugusa tukio hilo lililoamsha uzalendo na wakati huo huo kusababisha machungu mengi kwa wananchi wa Visiwa vya Zanzibar. Ninaamini kabisa kuwa kama Taifa wakati umefika wa kuirudia historia yetu kisomi na kisayansi na kuweza kutoa nafasi ya kuiandika kwa uwazi zaidi hasa kwa vile tuko mbali kidogo na matukio yenyewe lakini pia baadhi ya watu waliohusika bado wapo hai na wanaweza kutupa mwanga zaidi. Tutafanya makosa makubwa kama tuaendelea kuiogopa historia yetu kwa kisingizo cha “yaliyopita si ndwele”. Wasomi wetu na wanahistoria wetu waanze kazi ya kuiandika upya historia ya Taifa letu kwa ajili yetu sisi na wale wa vizazi vijavyo.

ZAHAMA LA MAFUTA: SERIKALI ITOE FUNDISHO Na. Jessica L. Fundi Jana tumeshuhudia mojawapo ya mambo ya kushangaza zaidi nchini na ya kutatiza vile vile. Kuna wafanyabiashara ambao walikula njama kusababisha upungufu wa bidhaa ya mafuta ya magari kwa kile ambacho wao waliamini kuwa ni kujaribu kuishinikiza serikali kuwaruhusu wauze mafuta hayo kwa bei yoyote ile bila kujali hali halisi ya soko, mahitaji, ugavi au upatikanaji wake.

Hawa wafanyabiashara kama walitaka kupinga agizo la EWURA walichotakiwa kufanya ni kwenda mahakamani kama walivyofanya Walimu au watu wengine ambao wanaona kuwa wameonewa. Vinginevyo wao wafanyabiashara wangeamua kuandamana ili tuwaone sura zao kuwa kweli wamechukizwa na

Walifanya makosa. Walijaribu kuiteka nchi nyara kwa kusababisha usumbufu usio wa lazima, lakini zaidi kwa kuingilia mtiririko wa shughuli za kiuchumi ambazo zinategemea sana usafiri unaotumia mafuta. Kosa hili ni lazima liwagharimu wafanyabiashara hawa ili liwe fundisho la kudumu. Liwe fundisho kuwa nchi yetu haiwezi kukaa katika huruma ya wafanyabiashara. Wengi wetu jana tumehangaika na kupoteza muda mrefu na wengine hata kupata ajali katika jitihada za kutafuta bidhaa hiyo ya mafuta.

kihuni na mimi kama mwanamama ninakilaani kabisa, kutokana na usumbufu na labda tushukuru kuwa imetokea siku ya mapumziko vinginevyo adha katika shule na sehemu nyingi za kazi isingekuwa mfano. Kama hili lilikuwa ni jaribio la kitu kikubwa zaidi, naisihi serikali ifute leseni za wale wote waliohusika na kitendo hiki na kuwafungia kabisa kushughulika na biashara ya mafuta vinginevyo walimwe faini kubwa ya kukumbukwa. Na zaidi ya yote wale waliopanga suala hili wafunguliwe mashtaka ya kuhujumu uchumi. Endapo serikali itakubali hawa wahuni warudie tena kitendo hicho, basi kweli nchi itakuwa imetekwa na mafisadi!

Foleni ya mafuta jana hilo la bei. Kitendo cha kuzuia bidhaa na hivyo kusababisha uhaba usio wa asili ni cha

Tuandikie mawazo yako kwa [email protected] (Attn: Jessica Fundi)

Soma bure

MOTO WA MABADILIKO UMEANZA...

Picha ya Wiki

KATUNI ZA WIKI

Wananchi walifunga eneo la Segera Michungani baada ya lori kugonga watu na kuparamia nyuma!

JIUNGE NA WANAKIJIJI WENZAKO!

http://www.mwanakijiji.com Jiandikishe kushiriki mijadala, kupata habari, kusikiliza muziki masaa 24 na matangazo ya moja kwa moja kila mwishoni mwa juma. Ukizungumzia habari, unatuzungumzia sisi!

K ut oka Hawa, jamaa wameanza kugoma ikiwa ni siku ya mapumziko na wakati wakuu wengi wako visiwa vya karafuu. Kama Dar hali ndiyo hivyo,sijui huko Kagera, Kigoma,Tabora,Rukwa,Songea na Lindi itakuwaje. Tulipiga kelele kipindi ambacho yule mama ZHM alipokuwa pale fedha kwa kuwatishia 'wakubwa" hawa nyau bila matendo. Mh! Ari mpya tuliiona,NGUvu mpya tuliiona sasa tuangalie KAsi mpya itakavyokuwa (ANGUKA) - Akajase Ukaidi wa hawa wauza mafuta lazima una sababu, haiwezekani amri ya serikali inayoheshimika ikadharauliwa na wafanyabiashara hivi hivi. Ni wazi wanajua hao viongozi wetu ni wadau katika biashara zao na ndio maana wanatutesa sisi walalahoi. Serikali ni lazima iwaonyeshe kuwa nchi hii ina utawala wa sheria ama sivyo tutasambaratika.—Bulesi Naishauiri serikali itafishe biashara ya mafuta. Enzi za Mwalimu hii mtu asingethubutu kufanya sabotage ya namna hii. Hawa ni sawa tu na wahu-

kw enye

m tand ao

jumu uchumi. Hawa ni wabaya kuliko EPA zote zilizowahi tokea nchi kwani wao wanamwumiza mwananchi papo kwa hapo. Nashindwa niseme nini ila nina chuki na hawa wahujumu au wahaini.— Ole Ndukai Kinachoniogopesha mimi mwenzenu ni tabia ya hawa wafanyabiashara ya mafuta kwani siku 1 mafuta yakipenda marekani wao wanapandisha bei ya mafuta siku hiyo hiyo lakini bei ya mafuta imeshuka kutoka dola 147 mpaka dola 47 tena kwa zaidi ya mwezi wao wanakataa kushusha bei inayolingana na kushuka; kwa nini? - Anon Kama ni kweli haya ndio yanaendelea, serikali inayowajibu wa kukagua hifadhi zao zote za mafuta kijiridhisha kwamba mafuta yapo ila wamekataa kuyauza then wawafungulie kesi ya kuhujumu uchumi.— Kichakoro Huku ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia. Lakini pia EWURA pia wanastahili lawama. Inaonekana hawakufanya homework yao vizuri. indicative prices ziko chini sana. Matokeo ndiyo haya.—Cynic

Cheche za Fikra

Mchapishaji na Mhariri Mtendaji M. M. Mwanakijiji Timu ya Waandishi Benjamin Mwalukasa— Mhariri Freddy Katunzi—Habari za Siasa Mahmoud Rashid—Habari mbalimbali Jessica L. Fundi – Makala Kwa kujiandikisha, maoni, habari, na ushauri Tuandikie: [email protected] Tovuti: http://www.mwanakijiji.com Kanusho: Mawazo yanayonukuliwa hayawakilishi msimamo au mawazo ya mchapishaji na utawala wa kijarida hiki.

Related Documents


More Documents from "Subi"