Toleojipya28

  • Uploaded by: Subi
  • 0
  • 0
  • December 2019
  • PDF

This document was uploaded by user and they confirmed that they have the permission to share it. If you are author or own the copyright of this book, please report to us by using this DMCA report form. Report DMCA


Overview

Download & View Toleojipya28 as PDF for free.

More details

  • Words: 3,794
  • Pages: 6
M O T O WA MA BA DI L I K O UM E ANZ A . . .

Cheche za Fikra

J U ZU U 7 TO LE O 28 F E B RU ARI 2 5 , 2 0 0 9

KIJARIDA CHA BURE— UKISHASOMA MPE MWINGINE—USIBANIE! MAKALA MAALUM

MRADI WA VITAMBULISHO

NINI HATUAMBIWI? SEHEMU YA II — TUUPINGE? Na. Fred Katunzi Katika toleo lililopita tumeelezea kwa kirefu teknolojia ya “smart card” na faida zake hasa inapotumika katika kutunza taarifa mbalimbali za mtu. Tulionesha kuwa ni teknolojia mpya, bora na ambayo bila ya shaka ina nafasi kubwa katika jamii yeyote ile kama inavyotumika tayari kwenye nchi mbalimbali kwa mambo mbalimbali. Hata hivyo katika toleo hili tujaribu kukushawishi mpendwa msomaji wa kijarida chako hiki ukipendacho kuwa mradi huu wa vitambulisho ambao tayari umeanza kutekelezwa ni

Kijarida Ulichoshika • Kinatoka kila Jumanne • Ni cha bure kabisa! • Kisichofungamana na chama chochote au fisadi yeyote!

Smart Card: Kama hii kutumika kama vitambulisho Tanzania mradi ambao kwa jinsi ulivyo umejengwa kwenye misingi mibaya, umeghubikwa na wingu kubwa la ufisadi, na utekelezaji wake unaonesha tangu mwanzo kabisa kuwa una matatizo mbeleni. Hata hivyo tuelewe kidogo mradi huu jinsi ambayo serikali

yenyewe inauelewa. Katika maelezo ya tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani http://www. moha.go.tz “Upembuzi yakinifu wa Vitambulisho vya Taifa ulikwishafanyika na matokeo ni kwamba Mradi unatekelezeka.” Tovuti hiyo inatoa taarifa kuwa tayari hatua za kuanza kuutekeleza mradi huo na kwa (inaendelea Uk. 2-4)

DR. DAU KUIOKOA BANDARI? Mamlaka ya Bandari Tanzania iko katika hali mbaya ya kiutendaji kiasi cha kuhitaji msaada wa dharura kama hali haiajafikia kubaya. Msaada huo yawezekana ukatokea pale Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya

Benjamin. G. Mwalukasa Mhariri

Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kuhamishiwa Mamlaka ya Bendera kwenda kuiweka sawa. Hadi hivi sasa jina la Dr. Dau linatajwa kuwa ni mtu pekee ambaye anaangaliiwa kupelekwa Bandari "kuinyosha" na

yeye mwenyewe kwa kweli inadokezwa kuwa yuko tayari kufanya hivyo. "Dau amefanya kazi nzuri NSSF na Rais amefurahishwa na sasa yuko tayari for the next assignment" kimetudokeza chanzo kimoja ambacho kimepitia uchambuzi wa majina ya waten-

• Kiko huru, kinathubutu, na hakiogopi mtu au hoja yoyote. • Ni kijarida chako! • Haki zote za kuchapa na kunakili zimeruhusiwa! Ndani ya Toleo Hili Juu ya Vitambulisho

1-4

Dau kwenda Bandari?

1,4

Mradi wa Vitambulisho

2,3

Hoja ya Mwanakijiji

4

Hoja ya Mwanakijiji

4

Da’ Jessy: Viongozi bora

5

Picha, Katuni na Maoni

6

UKURASA WA 2

CHECHE ZA FIKRA

VITAMBULISHO: NINI KINAFICHWA? namna nyingine basi hakuna kurudi nyuma. Unaweza kusoma taarifa ya Wizara kuhusu mradi huu kwenye tovuti yetu ya http://www.mwanakijiji.com Tovuti hiyo inaelezea kuwa kikao cha Baraza la Mawaziri cha Februari 2007 ndicho kilichoamua kuwa teknolojia ya “smart card” ndiyo itakayotumika kutekeleza mradi huu. Sababu kubwa pia zinazotolewa za kuwa na kitambulisho cha aina hiyo ni nyingi. Miongoni mwake ni kuwa kitambulisho cha taifa:



Kutambua mtu au mhusika.



Kusaidia kumtambua mhusika anapohitaji kupatiwa huduma katika Taasisi mbalimbali mfano benki,taasisi za mikopo, huduma za afya n.k.



Kuunganisha mifumo mingine kwa lengo la kuwasiliana na kubadilishana taarifa muhimu ambazo zitalenga kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji kuliko ilivyo hivi sasa.



Kumtambua mtu pale anapofanya uhalifu wa aina Fulani; hii itasaidia sana katika kupambana na uhalifu.



Kutambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye mabenki hasa pale wakopaji wanapochukua mikopo kutoka katika mabenki mbalimbali.









Kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari. Kutambua walipa kodi, hii itasaidia kupambana na wakwepaji wa kulipa kodi. Kumtambua mtu anapofanya biashara mbalimbali kwa kutumia majina tofauti. Kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii, kwa mfano kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu , haki za kujiunga na shule ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo Raia

wa Tanzania anastahili. Hii itasaidia kuondoa watumishi hewa kwenye “payroll “ ya Serikali.



Kuboresha utendaji kazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao; hasa pale wanapostaafu.



Kupunguza gharama za mwananchi kutokana na huduma mbalimbali anazozipata kutolewa na Taasisi moja.



Kurahisisha zoezi la kuhesabu watu/sensa.

Ni kutokana na haya yote ndipo tunaanza upingaji wetu wa mradi huu kama ulivyoelezwa na Wizara na ulivyofafanuliwa mara kadhaa Bungeni. UkiChiligati soma ukosoaji wetu utaona pia tunatoa mapendekezo yetu au fikra mbadala. Kipaumbele cha taifa ni nini? Kwa jinsi ambavyo mradi huu unapigiwa debe na kutetewa ni kana kwamba taifa letu liko kwenye hatari ya watu wake kutokujikutambua au kutambulika. Ni kana kwamba hadi hivi sasa hakuna jinsi ya kumtambua Mtanzania ni nani au hakuna jinsi ya kutunza kumbukumbu za mtu. Kuna haraka ya aina fulani ambayo bado haijaelezewa vya kutosha. Kuna ulazima gani na uharaka gani wa kukamilisha mradi huu sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote? Kwanini ipo hii haraka ya kutengeneza vitambulisho kwa gharama ya shilingi bilioni 200 (kwa kuanzia tu). Tukimuuliza Mkulima wa Ipinda, au mvuvi wa Mwaloni Mwanza au mchimba madini wa Geita hivi ni kitu gani unakihitaji katika maisha yako sasa hivi ni wangapi wataweka kitambulisho kuwa ni kitu cha kwanza? Jinsi inavyoonekana mradi huu umebuniwa na viongozi na ni wao pekee wenye kuushabikia. Kuna mambo mengine muhimu ya taifa ambayo yangestahili kupewa kipaumbele. Kwetu sisi tunaamini

kabisa kuwa kitu cha kwanza ambacho Tanzania inakihtaji hasa katika utendaji wa serikali ni udhibiti wa matumizi ya fedha za umma, kuziba mianya ya ufujaji, na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na wizi wa fedha za umma. Katika taifa ambalo tayari limepoteza karibu dola bilioni moja na ushee kutokana na uzembe na uongozi mbovu tutakuwa tunafanya makosa makubwa kuwapatia watu wale wale mamilioni mengine ya dola wakati tunajua kabisa kuwa hadi hivi sasa hakuna mtumishi hata mmoja wa ngazi za juu ambaye anatumikia kifungo kutokana na wizi, matumizi mabaya ya madaraka au ufujaji wa fedha za umma. Hivyo la kwanza kwa kweli ndilo hilo, kwamba katika mambo yote ya muhimu, ya lazima na yenye kuhitajika kitaifa, kweli kipaumbele chetu ni kuingia katika mradi huu wa “smart cards”? Vitambulisho vingine vipo tayari! Mtu anapozaliwa kuna cheti cha kuzaliwa, na kwa kadiri anavyoendelea anapata vitambulisho vya aina mbalimbali kuanzia vya shule, kazi, mahali n.k Na zaidi ya yote linapokuja suala la utaifa tayari kuna vitambulisho vinavyojulisha utaifa wa mtu pamoja na taarifa nyingine muhimu. Vitambulisho hivi vinaitwa “Pasi ya Kusafiria” yaani passport. Kwa mujibu wa maelezo ya Wizara vitambulisho vya taifa vitatolewa kwa mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18. Tovuti hiyo inasema kuwa “ni vyema ieleweke kwamba kadi za Vitambulisho vya Taifa zitatolewa kwa watu wazima kuanzia miaka 18 na sio watoto wadogo kama inavyoelezwa.” Sasa, ukituuliza sisi Cheche tutasema kwanini tusitumie utaratibu wa nchi kama Marekani au hata Uingereza ambapo ni rahisi kupata pasi ya kusafiria ambayo kimsingi ni kitambulisho cha mtu mwenyewe ambacho ndani yake kinabeba taarifa zake muhimu? Kama kuna haja ya kutumia smart card tunafahamu kuwa tayari pasi zetu zimeanza kutengenezwa kwa teknolojia mpya na hivyo kuongeza “smart card technology” haitakuwa jambo gumu.

KARIBU MWANAKIJIJI.COM

JUZUU 7, TOLEO 28

SAKATA LA VITAMBULISHO

Kwa vile pasi hizi zinatolewa kwa raia tu basi kwanini zisitumike pia kama vitambulisho ukizingatia mambo kadhaa.

shatumia gharama nyingi kama tukiangalia maneno ya mawaziri wa wizara hiyo miaka kama mitatu iliyopita.

-

Tayari lipo daftari (database) ya watu wenye pasi za kusafiria.

-

Tayari vipo vituo karibu mikoa yote ambapo watu wanaweza kuombea pasi hizo

-

Pasi ni vitambulisho vinavyoweza kumtambulisha Mtanzania akiwa ndani ya nchi yake au nje ya nchi.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Joseph Mungai (pichani) akizungumza kwenye Bunge la Bajeti la mwaka 2007/2008 alitoa taarifa ifuatayo kuhusu mradi huu: “Mheshimiwa Spika, katika Bunge la bajeti la mwaka wa fedha 2006/2007 nililiahidi Bunge lako tukufu kwamba baada ya kukamilisha zoezi la upembuzi yakinifu Wizara yangu ingeanza utekelezaji wa Mradi wa Vitam-

Kitu pekee ambacho naamini kinaweza kufanyika ni kubadili sheria yetu ili pasi zisiwe zinatolewa kwa sababu mtu anataka kusafiri kama ilivyo sasa bali ziwe ni haki ya raia na kila raia hata kama hana mpango wa kusafiri au kwenda nje ya nchi aweze kupata pasi hiyo. Mtindo huu ndiyo unatumiwa na nchi kama Marekani ambapo mtu mwenye “gamba la bluu” anajulikana ni Mmarekani na hakuna kitambulisho kimoja cha Taifa na hakuna utata wa Mmarekani kujijua au kujulikana ni nani. Tukumbuke pia kuwa Marekani ina watu zaidi ya milioni 300 na haina kitambulisho chenye mambo mengi kama hicho tunachokitaka Watanzania! Kimsingi tungeweza kufanya pasi ya kusafiria kuwa ndiyo kitambulisho cha kwanza (primary) kwa Mtanzania yeyote yule na ukweli wa mambo ni kuwa ndivyo tunafanya tayari, kwanini basi tusiongeze hivyo vikolombwezo vya teknolojia ya smart card kwenye pasi zetu? Gharama halisi haiko wazi Katika maelezo ya wizara, mradi huu wa vitambulisho utahusisha mambo mengi sana. Wao wenyewe wanasema kuwa mradi huu utagusa maeneo au idara angalau 10 katika kuufanikisha. Kuanzia TRA, RITA, TAMISEMI, Polisi n.k. Kwa watu wengi wanafikiri kuwa mradi huu “uta”gharimu shilingi bilioni 200. Siku chache zilizopita mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Gotham International ambayo ndiyo mshauri wa serikali kwenye mradi huu amenukuliwa na gazeti la serikali la Habari Leo akisema kwamba “mradi huo sio aghali kama nchini nyingine kwa sababu hakuna kitu kilichokwishafanyika bali taifa linaanza upya kwa kila eneo.” Ukweli ni kuwa tayari mradi wa vitambulisho ume-

UK.3

ya mshindi wa zabuni kujulikana! Pamoja na Mungai Waziri mwingine aliyetangulia kwenye wizara hiyo naye alitoa taarifa ifuatayo mwaka mmoja kabla na ndani yake kuna habari za kuzua maswali. Kapt. John Chiligati alitoa taarifa ifuatayo “Mheshimiwa Spika, sasa nieleze hatua tuliyofikia katika mradi wa kutoa vitambulisho vya kiraia. Tumemaliza hatua ya upembuzi yakinifu na tumeandaa mchakato (Action Plan) wa kuanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi huu katika mwaka wa fedha 2006/2007. Baada ya kupata baraka za Serikali, itaitishwa tenda ili kupata Kampuni yenye ujuzi na uwezo wa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa mradi huu. Maandalizi mengine ya kupata jengo la mradi na watumishi wa mradi yameanza kufanyika. Vile vile zoezi la kuwatambua wageni wanaoishi huko vijijini na mijini, na kuwaorodhesha limeanza katika Mikoa ya mipakani na baadaye litaendeshwa katika Mikoa yote Bara na Visiwani ikiwa ni mkakati wa kuzuia wageni wasipate vitambulisho vya Uraia hapo zoezi la kutoa vitambulisho litakapoanza.” Hapa napo tunaweza kuona kuwa tayari mradi huu umeanza kutekelezwa!

bulisho. Napenda kulijulisha Bunge hili kuwa Wizara imeanza utekelezaji wa mradi kwa kununua jengo kwa ajili ya Ofisi anzilishi ya mradi. Hali kadhalika Wizara yangu ikishirikiana na Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na Asasi nyingine zinaendelea na mchakato wa kuundwa kwa Wakala (Agency) itakayosimamia na kuendesha zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Taifa. Wizara inakamilisha Andiko la Maelezo ya Mradi (Project Design Document) ambalo ndiyo litatoa dira ya mwelekeo wa utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua. Aidha, zoezi la kuwatambua na kuwaorodhesha wageni wanaoishi vijijini na mijini linaendelea katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Mtwara, Mwanza, na Mikoa ya kati. Hii ni hatua muhimu ya maandalizi ya utoaji vitambulisho. Lengo la Serikali ni kukamilisha Mradi wa Vitambulisho ifikapo Desemba, 2009. Maana ya taarifa hiyo ni kuwa mradi huu tayari umeshatengenewa fedha, umeshapitishwa, na umeanza kutekelezwa! Haya yote yameanza kufanyika kabla hata

Angalia nayo maneno ya Waziri Mwingine aliyemfuatia Mungai Bw. Lawrence Masha naye anasema nini? Na yeye alitoa taarifa ifuatayo Bungeni mwaka jana “Mheshimiwa Spika, katika Bunge lako la bajeti la mwaka 2007/2008 nilitoa maelezo kuhusu maendeleo ya mradi wa vitambulisho. Napenda kuchukua nafasi hii kulijulisha Bunge hili kuwa Wizara yangu imekwisha karabati jengo la Ofisi anzilishi ya mradi na kumteua Mratibu wa mradi atakayesimamia shughuli zote za mradi.” Bw. Masha aliendelea “Aidha Wizara yangu ikishirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na asasi nyingine zipo katika hatua za mwisho za kuunda chombo kitakachosimamia na kuendesha zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Taifa. Katika hatua za awali za utekelezaji wa mradi Wizara yangu imekwisha tangaza zabuni ili kumpata mzabuni atakayejenga mfumo

Soma bure

UKURASA WA 4

CHECHE ZA FIKRA

DR. DAU KUIKOA BANDARI?

Vitambulisho mzima wa utunzaji kumbukumbu (data base) kwa nchi nzima. Hatua hii ni muhimu sana katika utekelezaji wa mradi, kwa kuwa kumbukumbu hizo ndizo zitatumika kutengeneza vitambulisho.” Kati ya Chiligati na Masha tunaweza kuona mambo kadhaa. Kubwa ni kwamba tayari zoezi la kuwajua wageni limeanza (kuanzia mikoa ya mipakani) na pia ofisi ya Maratibu imeshakarabatiwa. Hapa hatuna budi kujiuliza hizi fedha zote ambazo tayari zimetumika zimeidhinishwa kwa kupitia zabuni gani? Je hizi ni fedha za mradi huu huu na ni kati ya hizo bilioni 200 ambazo zinaombewa katika tenda au ni nje yake? Lakini ndani yake pia tunaona katika maneno ya Masha kuwa kuna tenda nyingine ambayo imetangazwa kwa ajili ya “kumpata mzabuni atakayejenga mfumo mzima wa utunzaji kumbukumbu (data base) kwa nchi nzima.” Sasa, labda kuna mtu atatupa maelezo kama zabuni ya vitambulisho ambayo tunaambiwa makampuni 6 yako kwenye mchakato wa mwisho ndiyo zabuni hiyo hiyo ya kutengeneza ‘database”? Kama siyo, hiyo ya database ni ya kiasi gani? Pia yapo maswali ya mahusiano ya baadhi ya makampuni ambayo tayari yako kwenye mchakato huu na baadhi ya viongozi ambao majina yao tayari tunayajua. Lakini zaidi ni kuangalia kama kuna njia mbadala za kutambulisha wananchi wetu bila kuingia mkataba huu mzito ambao kwa kila kipimo una wingu kubwa la maswali. Inaendelea wiki ijayo.

SWALI LA WIKI: Mradi wa Vitambulisho umeshaahirishwa karibu mara tatu sasa na hili linaloendelea ni mara ya nne kujaribu tena. Unafikiri mradi huu uendelee jinsi ulivyo ukisimamiwa na watu wale wale? Je ni mradi ambao unahitaji kuwa katika kipaumbele cha taifa zima? majibu yako: [email protected]

daji mbalimbali. Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo hicho kuna mabadiliko kadhaa ambayo yanaandaliwa na yatagusa ATCL, Tanesco, NSSF na Bandari hasa ukizingatia kuwa kati ya kampuni/mashirika hayo matatu ni moja tu ambalo linaonekana kuongozwa kwa manufaa (NSSF). Tuhuma dhidi ya Dr. Idris (TANESCO) na hili la Mattaka (ATCL) yamekuwa ni kizunguzungu kwa Rais kwani hawa ni watu wa karibu aliowaamini sana. "Mattaka anatafutiwa mahali pa kupelekwa na usishangae ukimuona anapewa ukurugenzi kwenye mojawapo ya mashirika makubwa ya umma" kimedokeza chanzo hicho. Kuhusu Dr. Idris chanzo kinasema kuwa endapo tuhuma dhidi yake hazitanasa (kama PCCB haitamshtaki) madhara yameshafanyika na anaweza kujikuta anapewa ubalozi mahali fulani. Mkurugenzi wa sasa Bandari Bw. Ephraim Mgawe (ambaye alikuwa ni Operations Manager chini ya Luhigo) inasemwa kuwa

hana uwezo wa kusimamia shirika hili na amekuwa ni kiini cha matatizo na kutokuwajibika na hana support ya wafanyakazi. Siku chache zilizopita baadhi ya makampuni yanayopitishia mizigo yao bandari ya Dar yameanza kutishia kuwa yataanza kutumia bandari ya Mombasa kwa ajili ya mizigo yao endapo huduma na hali ya bandari ya Dar haitatengemaa mapema. Hata hivyo siyo watu wote watafurahi kuona Dr. Dau akiondolewa NSSF na kwenda Bandari au shirika jingine wakiamini kuwa bado utaalamu na vipaji vyake vinahitajika kwenye shirika hilo hasa kutokana na usimamizi wa miradi mikubwa ambayo inawagusa Watanzania wengi. “Dau yeye pale pale NSSF amejitahidi kupatengeneza yafaa abakishwe pale PALE” mmoja wa watu wanaompigia debe abakie NSSF ametuambia. Hata hivyo licha ya hao wapo pia baadhi ya majina ya watu wengine wanaotajwa kuweza kwenda kujaribu kuokoa Mamlaka hiyo na baadhi yao bado majina yao hayajasikika sana kwenye kurasa za kitaifa. Miongoni mwao ni pamoja na Naibu Mkurugenzi wa sasa Bi. Happiness Senkoro na Kaimu Mkurugenzi usafiri wa majini Ndg. Funga Funga.

HOJA YA MWANAKIJIJI: BUNGE LITOE BARAKA BAADHI YA TEUZI Mara kadhaa tunasikia kuwa Rais amemteua mtu fulani kushika nafasi fulani na kuna wakati najiuliza kama kuna ulazima kwa Rais kufanya uteuzi mwingi namna hii. Kwa mujibu wa Katiba Rais anawateua watu wengi mno na uwezo wake huo wa kuteua kwa kiasi kikubwa hausimamiwi na chombo kingine na hivyo kufanya nguvu yake hiyo kuwa isiyo na kikomo. Ukiondoa uteuzi wa Waziri na Mwanasheria Mkuu nafasi nyingi ambazo ni nyeti katika Taifa zimeachwa mikononi mwa mtu mmoja kitu ambacho siyo sawa kwa demokrasia yetu hasa katika mfumo huu wa vyama vingi. Endapo chama kingine kitakuja kushika madaraka tunaweza kujikuta kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji lakini pia mabadiliko mengine ambayo yawezekana

yasiyo na ulazima lakini yakafanywa kwa sababu Rais anaweza. Hata leo kuna baadhi ya teuzi za Rais ambazo zimefanywa na zimegeuka kuwa kituko na hakuna mtu mwingine wa kumlaumu isipokuwa Rais mwenyewe. Ni Rais ndiye aliyemteua Mhe. Andrew Chenge kuwa Waziri wake (tena mara mbili) na ni yeye aliyemteua Bw. David Mattaka kuwa Mkurugenzi wa ATCL. Hivyo , tunapoona watu hawa wanaboronga wakati historia yao inajulikana kuna mtu mmoja tu wa kumlaumu naye ni yeye aliyewateua. Kwanini basi tusimpunguzie mzigo huu wa lawama?

JUZUU 7, TOLEO 28

UKURASA WA 5

N G U V U YA H O JA

TUNABURUZWA TU! Na. Bundukia

alio wateua na kuwa amini kuziongoza hawajui wakifanyacho, yeye ndiye anajua kila kitu hivyo inabidi awaelekeze wanatakiwa wafanye nini hasa.

Tatizo hili la maalibino kwisha kwake itakuwa ni kitendawili kikubwa kwani wanaongoza vita hii ni wanafiki. Hawalishuhulikii kwa dhati ya mioyo yao ila Angekuwa anayaona mauaji haya ni tatizo wanalishughulikia kwa vile inawalazimu angeyapa umuhimu hata basi kuiita wizara na wasipoonyesha kuwa wanafanya husika ya kwanza ili awape wahusika watawaliwa watauliza kulikoni. maelekezo yake nini cha kufanya. Hebu wananchi tujaribu kufikiria tuna waziri wa mambo ya ndani ambaye tatizo hili la mauaji ya alibino ndiye anayetakiwa kulishughulikia kwenye wizara yake. Lakini wapi bwana hivi karibuni wote tumemshuhudia hata kulitaja tu hatumskii yeye anahangaikia kujisafisha yeye na waliomteua ilikujitoa katika sakata la vitambulisho vya nchi lililowakalia kooni. Kwake yeye waziri haya mauaji ya alibino siyo suala zito; mara chache kumskia amelizungumzia hata kwa bahati. Mbaya zaidi hata Rais mwenyewe sina hakika sana kama analiona kuwa ni tatizo lenye uzito wowote katika kulishughulikia kwenye utendaji wake. Tumemuona hivi karibuni akirudia ule U-MR know it all wake wa kufanya zile ziara zake elekezi kwenye wizara (safari hii kwa kuwaita ikulu), kama vile wale

Ukiwasikia wanaongelea mauaji haya Wanasisa na viongozi watakuambia “wafanyabiashara ndio tatizo bwana”; sawa utafiti huu ambao ni wa kisanyansi mmeufanya wapi na lini ilikupata jibu hili rahisi? huambiwi. Kama mmegundua hivyo malizeni basi tatizo, wapi ndio linaendelea. Inawezekana hawa viongozi ndio wahusika wakuu na ndio maana wanasutwa na nafsi zao. Tunasema hivyo kwa sababu hatuoni umakini wowote katika kulishughulikia na kulitafutia ufumbuzi. Tunachokishuhudia ni jitihada za kukurupuka katika kushughulikia kila tatizo la nchi hii. Utasikia leo wamegusagusa EPA, kesho SAGEM SECURITE, kesho kutwa Twin Tow-

ers n.k yaani ni vurugu mechi tupu. Unasikia Rais kaunda kikosi kazi, wajumbe, Mataka yuko ndani, kipofu aliyeshidwa kuliongoza shirika lake akawasaidie vipofu wezake! Hatuko makini! Sasa kwa kufanya hivi sijui anamkomoa nani wale wanao jaribu kupinga maamuzi yake au yeye mwenyewe pale tutakapoanza kumuuliza fedha za walipa kodi alizowagawia kiholela kama za kutoka mfukoni kwake zimelisaidiaje shirika la ATCL. Tufike mahali tuwe hatuna budi (tulazimike basi) kuuwekea wasiwasi uwezo wa Rais wetu. Hivi pale chuo kikuu kuna mtu anaweza kutueleza kuwa alitoka na pass mark gani? hivi huyu ana washauri wenye uwezo gani? je anawasikiliza kweli washauri wake wanapompa ushauri wa kitaalamu au ndio hivyo ni U -MR know it all kwenye kila jambo? Kama anawasikiliza na kutekeleza anayoshauriwa basi yeye na hao wanaomshauri watakuwa wana matatizo makubwa na hawawezi kutuongoza wameshindwa kazi waliyopewa na Watanzania. Watutangazie na tufahamu hivyo na sisi tutafute nini tukifanye kuondokana na matatizo haya ifikiapo 2010.

DA’JESSY: VIONGOZI WAFANYE MAAMUZI MAGUMU Na. Jessica L Fundi Naamini sifa moja ya kiongozi ni uwezo wake kuona tatizo, kulichambua, kupima uzito wake na kuangalia njia za kulikabiri. Kiongozi mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kuona njia zaidi ya moja ya kulikabili tatizo na katika njia hizo zote anao uwezo wa kuona njia inayofaa, yenye gharama nafuu, na ambayo inahakikishia matokeo bora zaidi. Kiongozi ambaye hawezi kufanya mambo hayo anabakia kuwa ni kiongozi wa jina tu. Katika kufikia hatua hiyo ya kuweza kuchagua njia iliyo bora kukabiliana na matatizo au changamoto mbalimbali, kiongozi mzuri basi ni yule

mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Maamuzi ambayo yanaweza kuwaudhi rafiki zake na kumgombanisha na ndugu zake, maamuzi ambayo jamii kubwa yaweza wasielewe. Ni jukumu la kiongozi huyo basi kuweza kuwashawishi wananchi au wale anaowaongoza kwamba ni kwanini mambo fulani yanafanywa au yanapangwa kufanywa, na kwanini ni lazima yafanywe jinsi yatakavyofanywa. Hivyo basi kiongozi haogopi au hakwepi shutuma, kejeli, au mapingamizi. Bali huyakumbatia, na kwa umahiri mkubwa kuyapangua moja baada ya jingine nahivyo kufanya hoja yake ikubaliwe na kupokelewa na watu wengi zaidi. Katika kufanya maamuzi magumu basi kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo siyo wa

kukubali tu bali uwezo wa kukataa; uwezo na ujasiri wa kusema hapana. Naamini taifa letu linatafuta kiongozi au viongozi ambao wanaweza kusema jambo hili hapana na wakasimama hivyo ingawa yawezekana msimamo huo waweza kuwajengea uadui au kuleta mgongano na wa wetu wengine. Kiongozi wa aina hiyo ni kiongozi ambaye atasukumwa kweli na maslahi ya taifa na ya wananchi wenzake na kwake yeye kitu kingine nje ya hicho hakina nafasi. Ninavyoangalia mambo yanavyoendelea najiuliza kama siku moja tutakuwa naye! Yaani kiongozi mwenye ujasiri wa kufanya maamuzi magumu! Email: [email protected]

MOTO WA MABADILIKO UMEANZA...

Picha ya Wiki

KATUNI ZA WIKI

Mzee Butiku akikaribishwa kwenye Mkutano wa CUF (picha kwa hisani ya Mpoki)

PATA HABARI MOTOMOTO NA MIJADALA

http://www.mwanakijiji.com Jiandikishe kushiriki mijadala, kupata habari, kusikiliza muziki masaa 24 na matangazo ya moja kwa moja kila mwishoni mwa juma.

Ukizungumzia habari, unatuzungumzia

K ut oka Ukiona nchi inababaika na kutapatapa, jua uongozi hakuna na CCM inababaika kwa sasa kwa sababu hakuna uongozi. – Butiku Sasa hivi (mafisadi) wameanzisha magazeti, nawaomba muwapuuze na tusonge mbele katika vita yetu hii ambayo mwisho wake ni kuondoa umaskini nchini—Dr. Mwakyembe Ile dhana kuwa wazee ni dawa sasa haipo, kumbe wazee wengine ni sumu, kweli mizizi ni dawa, lakini mizizi mingine ni sumu, mzee wetu huyo ambaye CCM na wana-CCM tunamheshimu sana, ametudhihirishia hivyo— Amos Makalla akimjibu Butiku Nakumbuka Pengo alivyokuwa critical kwa serikali ya Mwinyi, nami nilikubaliana naye kwa kiasi kikubwa kwani kuna mambo ambayo nafikiri yalikuwa yakifanyika kinyume na ilivyotakiwa yafanyike na nikamuona kama shujaa. Inaniuma sana shujaa wangu anapogeuka na kuaangalia tu mafanikio ya kanisa lake. Hivi ni amani ipi anayoi-

kw enye

m tand ao

hubiri katika taifa ambalo majambazi kabla ya kukamatwa yanaandaliwa makao keko yanayolingana na hadhi zao kwa gharama za mlipa kodi anayelazimika kulala kitanda kimoja na mgonjwa mwenzake wodini kwa kuwa vitanda havitoshi? - Gagnija Bahati mbaya wafu hawasemi, kama wangekuwa wanasema Mwalimu angekataa kata kata Mkapa kutembelea kaburi lake lakini familia ya Mwalimu inaweza kabisa kufanya hivyo kwa niaba yake.—Bubu Ataka Kusema Membe na lowassa wanatoana jasho kwenye mradi wa vitambulisho, MEMBE kafanikiwa kupata tenda ya mradi huu kwa kushikiana na Mwikalo,cha ajabu mradi wenyewe ni bilioni 72 lakini kina MEMBE wamepeleka kuwa bilioni 220 ili wapate pesa za kampeni za urais 2015. Inatakiwa MEMBE achunguzwe na kampuni ya mjukuu wa nyerere Jack Gotham nayo ichunguzwe. – Msema Kweli

TOA NAKALA MOJA

Cheche za Fikra

Mchapishaji na Mhariri Mtendaji M. M. Mwanakijiji Timu ya Waandishi Benjamin Mwalukasa— Mhariri Freddy Katunzi—Habari za Siasa Mahmoud Rashid—Habari mbalimbali Jessica L. Fundi – Makala Kwa kujiandikisha, maoni, habari, na ushauri Tuandikie: mhariri@ klhnews.com Tovuti: http://www.mwanakijiji.com Kanusho: Mawazo yanayonukuliwa hayawakilishi msimamo au mawazo ya mchapishaji na utawala wa kijarida hiki.

Related Documents

Toleojipya28
December 2019 30

More Documents from "Subi"