M O T O WA MA BA DI L I K O UM E ANZ A . . .
Cheche za Fikra
J U ZU U 6 TO LE O 21 J AN U A RI 0 6 , 2 0 09
KIJARIDA CHA BURE— UKISHASOMA MPE MWINGINE—USIBANIE!
MAUAJI YA ALBINO
USALAMA WA TAIFA YAINGILIA KATI habari zozote ambazo zinahusiana na masuala ya usalama wa Taifa na ambazo zina umuhimu katika kudumisha utulivu na usalama nchini imesambaza maafisa wake sehemu mbalimbali nchini kuanzia mwishoni mwa mwaka 2008.
Rashid Othman—Mkurugenzi wa TISS
Na. Fred Katunzi Idara ya Kijasusi ya Tanzania (TISS) kwa namna ya pekee na kwa makusudi imeunda timu maalum za kufuatilia mauaji ya Watanzania wenye upungufu wa
chembe za kuzalisha rangi mwilini yaani ulemavu wa Ualbino.
“Ndiyo, tuna maafisa wetu ambao sasa hivi wako “field” wakishirikiana na Polisi kukusanya taarifa za kijasusi” alisema mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa TISS akizungumza na kijarida hiki masaa machache Tuna maafisa wetu kabla ya ambao sasa wako “field” kufunga mwaka 2008.
Taarifa za kuaminika toka ndani ya serikali zimeimbia “Cheche za Fikra” kuwa taasisi hiyo ambayo inajukumu la kukusanya
Kuundwa kwa (inaendelea Uk. 2)
Benjamin. G. Mwalukasa
Kijarida Ulichoshika • Kinatoka kila Jumanne • Ni cha bure kabisa! • Kisichofungamana na chama chochote au fisadi yeyote! • Kiko huru, kinathubutu, na hakiogopi mtu au hoja yoyote. • Ni kijarida chako! • Haki zote za kuchapa na kunakili zimeruhusiwa!
Ndani ya Toleo Hili
HOJA YA MWANAKIJIJI — CHADEMA WAMEZEMBEA MBEYA?
Usalama wa Taifa
Heri ya Mwaka Mpya!2009! Mojawapo ya mambo ya kushangaza yaliyotokea hivi karibuni ni jinsi gani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakitasimamisha mgombea katika kinyang’anyiro cha cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
kilichotokea na kuwa huko mbeleni kuna haja yakujifunza zaidi.
Hoja ya Mwanakijiji
1
Hoja ya Mwanakijiji
2
Nini hasa kilitokea Mbeya Vijijini hadi kusababisha Chadema kutokuwa na mgombea?
Hoja ya Mwanakijiji
3
Jessica: Jando & Unyago
3
Baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe. Richard Nyaulawa,
Maoni ya Mtandao
4
Picha na Katuni
4
Nimepata nafasi kuulizwa mas-
wali mengi na watu mbalimbali na wengi wametaka kujua maoni yangu kuhusu suala hili lilivyo na ninachukuliaje jambo hili. Nimeandaa hoja yangu leo kwa mtindo wa maswali na majibu na ni matumaini yangu majibu yangu tayachangia kidogo tu katika mjadala wa kile
1, 2
PAGE 2
CHECHE ZA FIKRA
TISS YAINGILIA KATI MAUAJI YA ALBINO Timu hizo kulithibitishwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya kuaga mwaka 2008 kwa Taifa. Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alielezea mkakati wa serikali yake kupambana na uhalifu huu ambao mwaka jana umeshuhudiwa Maalbino zaidi ya thelathini wakiuawa kwa kunyofolewa viungo vyao na wengine ambao walikuwa wamekufa kwa sababu mbalimbali makaburi yao kufukuliwa na miili yao kukufuriwa (desecration) kwa kunyofolewa viungo. Rais Kikwete alisema kuwa “tumeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya. Hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.” Tulipomuuliza afisa huyo ni kwanini TISS imeunda kikosi hicho sasa wakati mauaji haya yameendelea kwa muda wa karibu mwaka mzima alisema kuwa “tumekuwa tukitoa msaada kwa Jeshi la Polisi lakini mara zote tumewaacha wao waongoze uchunguzi huu” Afisa huyo aliongeza kwa kusema kuwa “kwa kadiri siku zilivyoendelea ndivyo tulivyogundua ni jinsi gani Jeshi la Polisi halina
uwezo wa kukusanya taarifa za kijasusi na kuweza kuzifanyia kazi”. Afisa huyo alitolea mfano tukio lililotokea siku chacha baada ya Krismasi huko Mkoani Pwani ambapo mama mmoja na mwanawe mkubwa wa kiume walikula njama ya kumuuza binti yake kwa shilingi milioni 15. Binti huyo ana ulemavu wa ngozi. “Mama huyo Mwajabu Said na mwanawe Saidi Omari walikubaliana na watu Magazeti hayawasiojulikana kumuuza Kabuyu Dalili (22).” Afisa huyo alisimulia kisa hicho. yanahaririwa na
wahariritaarifa wale alienda wale “Sasa yule binti alipopata Polisi na wao polisi badala ya kuweka mtego wa kwenda kuwakamata hadi wanunuzi, wao wakamuacha binti kituoni na kwenda kuwakamata yule mama na mwanae na hivyo kuvurunda uchunguzi” alisema afisa huyo. Kwa mujibu wa ofisa huyo wa TISS dalili zote zinaonesha kuwa kuna kikundi cha watu wachache ambao ndio wanaratibu biashara hii haramu na mtandao wao umejikita kwenye maeneo ya kanda ya ziwa. “Cha kushtua zaidi ni kuwa matukio mengine ya mauaji ya Albino ni ya kuiga (copycats) ambapo baadhi wa “waganga”
sehemu nyingine nchini wamekuwa wakitoa maagizo hayo ya kutaka viungo vya Maalbino baada ya kusikia kuna watu wanaamini mambo hayo na wako tayari kulipa mamilioni.” alisema ofisa huyo ambaye anafahamu kwa undani jukumu lililoko mbele yao. Wakati huo huo, wakati wowote mapema mwaka huu serikali imeandaa mpango wa kura za maoni kwa nchi nzima kuhusu taarifa za watu wanaojishughulisha na mauaji haya. Hilo lilisemwa na Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa Hata hivyo afisa aliyezungumza nasi ameelezea kuwa na maswali na mpango huo akidai kuwa unaweza kusababisha “kusakana uchawi (witch hunting) na watu wanaweza kutajwa kwa sababu za chuki na kisasi”. Mauaji ya Albino yamefanyika pia nchini Burundi ambapo hadi mwezi Septemba mwaka jana watu sita walikuwa wamuawa. Kijarida cha Cheche kinaendelea kupinga na kulaani vikali vitendo hivi vya mauaji ya Albino kuwa ni vya kinyama, na visivyo na nafasi katika Tanzania mpya tunaoijenga.
HOJA YA MWANAKIJIJI: CHADEMA ILIVYOZEMBEA vyama vya kisiasa vilifahamu fika kuwa kutafanyika uchaguzi mdogo, ambao kwa mujibu wa sheria ulitakiwa uwe ndani ya siku tisini tangia nafasi hiyo iwe wazi. Vyama vilianzisha michakato ya kutafuta wagombea wake na Chadema ilimpata mgombea wake Bw. Shabwee Shitambala. Hata hivyo kabla ya kuanza kampeni na mambo mengine kuelekea uchaguzi ni lazima fomu zote za wagombea zipitiwe na msimamizi wa uchaguzi na zinakuwa wazi kwa wagombea wengine kuziangalia. Wagombea wa CCM na CUF waliona kuwa fomu za Shitambala zinaonesha kuwa aliapa kupitia kampuni ya uwakili badala ya Mahakama ya mwanzo, wilaya, n.k kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya 1985. Kutokana na hilo wagombea wa CUF na CCM walimuwekea pingamizi mgombea huyo wa
Chadema, pingamizi ambalo lilikubaliwa na msimamizi wa uchaguzi Bi. Juliana Malange. Chadema walijaribu kukata rufaa kwa Tume ya Uchaguzi na siku ya Ijumaa iliyopita Tume hiyo ikiwa na majaji wanne waliitupilia mbali rufaa hiyo wakikubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa uchaguzi na hivyo kuiweka Chadema nje ya kinyang’anyiro hicho ambacho kwa watu wengi kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu kuona mpambano mwingine kati ya Chadema Vs. CCM baada ya ule wa Tarime ambapo Chadema iliibuka kidedea. Je lililotokea ni jambo dogo? La hasha. Kilichotokea Mbeya vijijini ni jambo kubwa na zito. Ni jambo ambalo limeikosesha Chadema nafasi ya kujipima kwenye uwanja wa ugenini. Kushinda Tarime ilitarajiwa. Mara mbili
wamepata nafasi ya kujipima ugenini na mara zote wameshindwa kufurukuta (kwa sababu mbalimbali ambazo wao wanazo). Walipata nafasi Tunduru, walipata nafasi Kiteto. Kwanini ni muhimu kushinda ugenini? Kuanzia mwaka juzi wakati wa sakata la Buzwagi, Chadema wanaamini kuwa wanakubalika zaidi na wananchi sehemu mbalimbali nchini. Lakini vilipokuja vipimo vya sanduku la kura hawakufanya vizuri. Kukubalika kwa chama cha kisiasa siyo maandamano au makusanyiko ya watu; siyo kusifiwa kwenye mitandao au kuandikwa magazetini. Kipimo cha kukubalika kwa chama cha kisiasa ni kwenye sanduku la kura. Baada ya watuhumiwa wa ufisadi kufikishwa mahakamani na kati yao wapo
KARIBU MWANAKIJIJI.COM
JUZUU 6, TOLEO 21
PAGE 3
HOJA YA MWANAKIJIJI
waliokuwa kwenye ile orodha ya mafisadi; na ile nyaraka ya kina Jeetu, basi Chadema ilikuwa ni jimbo la Mbeya Vijijini kujipima kama kweli wanakubalika. Hadi Chadema iweze kushinda ugenini kwa kutumia hoja (siyo mtu wanayemsimamisha) bado hakijafanya kitu cha ajabu katika sanduku la kura.
Hivyo Mbeya Vijijini kwa maoni yangu lilikuwa ni jimbo la Chadema kulipoteza na CCM kulishikilia tena. Sasa wangepoteza kwenye sanduku la kura tungeweza kupima mikakati yao, hoja zao n.k lakini kupoteza kwa kushindwa kufuata taratibu ambazo zinajulikana hicho ni "kilele cha uzembe". Hilo ni kosa tu mwanakijiji, na makosa yanatokea? Hapana kilichotokea siyo kosa; makosa ni kitu ambacho hakiko ndani ya uwezo wako kujua, kujiandaa au kwa namna yeyote ile kutarajia. Makosa ni kitu ambacho kinatokea na kiko nje ya uwezo wako na kikitokea unajua hutarudia tena (ndiyo msemo wa "kutenda kosa si kosa"). Kilichotokea ni kuboronga, kuvurunda,
kuharibu! Nikiandaa fomu inasema "Jina la Kijiji" na
wewe ukaja ukaandika "Mkoa wa Tanga". Ulichofanya siyo kosa, ni kuvurunda hasa kama wewe ni mkuu wa mkoa! Yeyote anayegeuza hili kuwa ni jambo la kosa tu, ameshindwa kupima uzito wa kilichotokea; hakikupaswa kutokea, hakina udhuru isipokuwa kukubali tu kuwa hapo walichemsha na kutoka hapo kusonga mbele. Lililotokea Mbeya linaonesha jinsi Chadema isivyo chama Makini na hawastahili kuaminiwa zaidi sivyo? Hapana, tukiamua kuweka kuboronga kwa Chadema Mbeya Vijijini na kuboronga kwa CCM kitaifa na tukavipima
kwenye mizani, wala havikabiribiani. Kilichotokea kwa Chadema kinawaathiri wao zaidi lakini hakilipi Taifa hasara yoyote ile zaidi ya fedheha kwa uongozi wa Chadema. Kilichofanywa na CCM na serikali yake siyo kilele tu cha uzembe bali ni utawala wa uzembe. Sitaki kurudia mifano; Serikali ya CCM iliboronga mkataba wa IPTL, mkataba wa Richmond, TRL, Tanesco, na sasa TRL na ATCL. Hayo yote ni mambo ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wao kuyasimamia. Tukio la Chadema kuvurunga kuapishwa kwa mgombea wao kabla ya uchaguzi mdogo na mlolongo wa matukio ya serikali ya CCM kuuza raslimali zetu kama njugu za bure havilingani hata kidogo kwa uzito wake. Yeyote anayeihukumu Chadema kana kwamba ni chama tawala si mkweli kwa historia wala nafsi yake. Kuhusu kuaminiwa hili linategemea kuwaamini katika nini. Niliwahi kuandika mada katika jamii forum miaka karibu mitatu iliyopita inayosema “Wapinzania ni wakombozi”? NIlielezea kwa kirefu kusita kwangu kuweka tumaini langu kwa vyama vya upinzani. (Itaendelea wiki ijayo)
DADA Jessy: WATOTO WETU WANAFUNZWA NA NANI? Na. Jessica L. Fundi Kuna mambo matatu yametokea siku za hivi karibuni ambayo yamenifanya nijiulize kama ninafanya kila niwezalo kumfunza binti yangu katika maisha mema na ya maadili mazuri. Kuna wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT (Mt. Augustino Nyegezi) ambao wamesimamishwa/kufukuzwa baada ya picha zao walizojipiga wakiwa watupu (na nguo za ndani tu) kusambaa kwenye mtandao. Labda ndio uzee au ushamba wenyewe lakini sijaelewa bado kwanini binti msomi unayejijua thamani yako ukapiga picha za aina hiyo ambazo zimegharimu ramani ya maisha yako? Jambo jingine ni hili ambalo nimeanza kulisikia siku chache zilizopita kuwa Rais Kikwete inasemekana amemcheza mtoto wake wa kike katika kile ambacho kinasemwa kuenzi mila na desturi za Kikwere.
Jambo la tatu lilitokea wiki chache kabla ya siku kuu ya Krismasi ambapo nilialikwa kwenye “kitchen party” ambapo niliyoyaona na kuyasikia mengine sijui yanatoka sayari gani!
ndoa na familia. Sasa leo hii katika ulimwengu huu wa teknolojia ambao habari zinasafiri kwa haraka kuliko wakati mwingine wowote na siri za vyumbani siyo siri tena tunaweza vipi kama jamii kuwaandaa watoto wetu wa kike na wa kiume kuingia maisha ya ujana na utu uzima?
Haya yamenifanya nijiulize kweli? Enzi za wazee wetu tulikuwa na mambo ya ya Jando na Unyago ambapo watoto wa kike na wa kiume waliofikia balehe wanafundishwa mambo mbalimbali Je tutaendelea kuziachia filamu, intaneti, na hususan ya jinsia zao na pia kuandaliwa porojo za mitaani kuendelea kuwafunza maisha ya kiutu uzima. watoto wetu? Vinginevyo tufanye nini kuwaandaa watoto wetu kwa maisha ya utu Lengo la mafunzo hayo ya kijadi lilikuwa uzima? kumsaidia kijana kutoka maisha ya utoto kuingia ujana na hatimaye kuwa tayari Je ipo haja ya kuangalia ni jinsi gani mambo kuingia maisha ya utu uzima. ya unyago yanaweza kurudishwa katika ulimwengu wetu mambo leo? Mafunzo hayo ya jadi yalisaidia sana kuiandaa jamii licha ya ukweli kwamba Tuandikie mawazo yako kwa baadhi ya mafundisho ni ya kizamani na
[email protected] (Attn: Jessica Fundi) ambayo yanapingana na uelewa wetu wa kisayansi ya zama hizi. Hata hivyo, mafunzo yale yalibakia kuwa njia ya kuwaandaa watoto wa kike (na wa kiume) katika maisha ya
Soma bure
MOTO WA MABADILIKO UMEANZA...
Picha ya Wiki
KATUNI ZA WIKI
Ijumaa 2 Januari, 2009, Waislamu wa Tanzania waliandamana kupinga uvamizi wa Israel kwenye Ukingo wa Gaza
JIUNGE NA WANAKIJIJI WENZAKO!
http://www.mwanakijiji.com Jiandikishe kushiriki mijadala, kupata habari, kusikiliza muziki masaa 24 na matangazo ya moja kwa moja kila mwishoni mwa juma. Ukizungumzia habari, unatuzungumzia sisi!
K ut oka (ATCL) Wasipewe pesa tu za walipa kodi kama vile kuna kisima cha kuchota. Jingine wamewawezesha vipi au watawawezesha vipi ili kununua ndege mpya za kisasa? Kuweza kufanya ushibdani kwenye safari ambazo zina faida kubwa? Kwa sababu wanakurupuka kila baada ya miaka miwili watakuwa wanatoa pesa nyingine - Hivi kweli hatuna walio na uchungu na hii nchi? Dua Hii pesa imetolewa iliwe au ndio mikakati ya kuanza kukusanya pesa ya uchaguzi . Kweli pesa ya "bail-out" inatolewa kisha ndio inaundwa kamati ya kutambua matatizo ya shirika! Mimi nilidhani "bail-out" ni kukwamua kutoka matatizo sasa kama hayo matatizo huyajui una"bail-out" nini? yale yale ya reli.– Duru Langu Hivi karibuni tumeshuhudia Yona, Mramba na Mgonja wakijiwekea dhamana kwa kutumia baadhi ya mali zisizohamishika, zenye thamani kubwa ya fedha - mabilioni.Hawa viongozi hawana background ya biashara, ni kweli
kw enye
m tand ao
kwa savings za allowance za serikalini wameweza kukusanya utajiri mkubwa kiasi hicho? - Kinetiq01 Mwaka huu tutasikia na kuona mengi sana sana....sijui atabakia nani huko serikalini maana mmm wote karibu wachafu jamani sijui hata mkuu wa kaya kama atakoswa angalau kutajwa tu maana nae yumo jahazini tangu 1988...IPTL sidhani kama itamkosa.....yangu macho na masikio— Skills4ever Kwa kweli cheche inatisha(wananchi wanaikubali vilivyo) Katika moja ya vyuo vikuu hapa nchini,jana nilishuhudia dr. (lecturer) akitumia zaidi ya dakika 5 kutuelezea wanafunzi uzuri wa cheche! amazing wanafunzi wote walikuja juu kutaka kujua ni jinsi gani watakavyopata kijarida cha cheche.— J.J.
Cheche za Fikra
Mchapishaji na Mhariri Mtendaji M. M. Mwanakijiji Timu ya Waandishi Benjamin Mwalukasa— Mhariri Freddy Katunzi—Habari za Siasa Mahmoud Rashid—Habari mbalimbali Jessica L. Fundi – Makala Kwa kujiandikisha, maoni, habari, na ushauri Tuandikie:
[email protected] Tovuti: http://www.mwanakijiji.com Kanusho: Mawazo yanayonukuliwa hayawakilishi msimamo au mawazo ya mchapishaji na utawala wa kijarida hiki.