Cheche Za Fikra, Toleo Na. 19

  • Uploaded by: Subi
  • 0
  • 0
  • December 2019
  • PDF

This document was uploaded by user and they confirmed that they have the permission to share it. If you are author or own the copyright of this book, please report to us by using this DMCA report form. Report DMCA


Overview

Download & View Cheche Za Fikra, Toleo Na. 19 as PDF for free.

More details

  • Words: 2,452
  • Pages: 4
M O T O WA MA BA DI L I K O UM E ANZ A . . .

Cheche za Fikra

J U ZU U 5 TO LE O 19 DI SE M BA 2 3 , 2 0 0 8

KIJARIDA CHA BURE— UKISHASOMA MPE MWINGINE—USIBANIE!

BENKI M ICHUNGUZWE —1 hii ni kuonekana kwa baadhi ya majina ya watu ambao wanahusishwa na wizi wa EPA na ambao wengine wameshafikishwa mahakamani katika kile ambacho wachunguzi wa mambo ya kisheria wanakiona kama jaribio la kupambana na vitendo vya kifisadi nchini.

Mtoto Albino

Majengo ya Benki Kuu Makao Makuu mjini Dar

Na. Fred Katunzi

taasisi nyingine ambazo tutazitaja hapa zinatakiwa kufanyiwa uchunguzi huru na wanahisa wake kuchunguzwa ili kuona uhusiano uliopo wa

Mojawapo ya taasisi ambazo kijarida chako cha “cheche” kinaamini inatakiwa kusimamishwa mara moja na kuanza Tunafikiria sheria ya kufanyiwa uchunguzi wa kuhusika na “Proceeds of Crime” ya uhalifu ni Benki M am1991 bayo ilianzishwa miaka michache iliyopita na kuanza kujipatia umaakuundwa kwa Benki hiyo na rufu mkubwa katika medani wizi wa mabilioni ya fedha kuza shughuli za kibenki toka Benki Kuu ya Tanzania nchini. mwaka 2005/2006 na kabla yake. Tunaamini kuwa Benki M na Kilichotushtua kuhusu Benki

Tunayaandika haya tukiifikiria sheria ya “Proceeds of Crime” ya mwaka 1991 ambayo tunaamini endapo itafuatwa kama inavyotakiwa kufuatwa tuna uhakika msululu wa watu kutiwa pingu una orodha ndefu ya watu ambao hadi hivi sasa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Wahusika wakuu wa Bank M Ili kuweza kuelwa msimamo wa “Cheche” leo kwanini tunataka Bank M isimamishwe na kufanyiwa uchunguzi mara moja ni wahusika waliomo kwenye Bank M wanahusika moja kwa moja na baadhi ya malipo ya ajabu kabisa na wizi wa wazi kwenye Benki Kuu. Watu hao hawakupaswa kabisa kufungua Benki yoyote nchini hata kwa kisingizio cha “uzalendo”. Lakini zaidi (Inaendelea Uk. 2)

Benjamin. G. Mwalukasa

Kijarida Ulichoshika • Kinatoka kila Jumanne • Ni cha bure kabisa! • Kisichofungamana na chama chochote au fisadi yeyote! • Kiko huru, kinathubutu, na hakiogopi mtu au hoja yoyote. • Ni kijarida chako! • Haki zote za kuchapa na kunakili zimeruhusiwa!

Ndani ya Toleo Hili

HOJA YA MWANAKIJIJI — HERI YA SIKU KUU YA NOELI!

Benki M na wizi BOT -1

1, 2

Kwa niaba yangu, waandishi na wasomaji wa kijarida chenu mkipendacho cha “Cheche za Fikra” tunapenda kuwatakia ndugu zetu Wakristu mahali pote duniani heri ya Siku Kuu ya Kuzaliwa Bw. Yesu Kristu.

Hoja ya Mwanakijiji

1

Benki M na wizi BOT

2

Hoja ya Rev. Kishoka

3

Picha ya wiki

4

Tunawatakia pia mapumziko mema wasomaji wetu wote! M. M. M.

Maoni ya Mtandao

4

Katuni

4

PAGE 2

CHECHE ZA FIKRA

BENKI M NA WIZI WA BOT—1 ni jinsi gani kuanzishwa kwa Bank M kunaihusisha serikali ya Rais Mkapa na tuna uhakika wa asilimia 100 kwamba Rais mstaafu alijua au alipaswa kujua juu ya waanzilishi wa benki hiyo kwani ni yeye aliyewapangisha jengo lao la kwanza pale barabara ya Ocean Road karibu kabisa na makazi yake rasmi. Jeetu Patel Wengi wameshalisikia jina la bwana huyu ambaye hivi sasa amesimamishwa kizimbani kwa tuhuma za wizi wa mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya EPA. Bw. Jeetu Patel. Wakati wa uanzishwaji wa Bank M Bw. Patel na wenzake (akiwa mshtakiwa mwingine Devendra Patel) walikuwa na hisa za Shilingi bilioni 1.3 kwenye benki hiyo. Tatizo ni kuwa wakati wanajiandikisha kwenye kampuni hiyo inadaiwa tayari walikuwa wameshachota fedha za EPA kiasi cha shilingi bilioni 10! “Hizo fedha walizozileta kwenye Benki M ni kutokana na hizo fedha za EPA” amesema afisa mmoja wa usalama ambaye amekuwa akifuatilia kesi hii kwa karibu na ambaye ametilia msisitizo wa watuhumiwa vigogo zaidi kufikishwa mahakamani. Uchunguzi unaonesha kuwa hadi mwaka 2005 Bw. Patel na kundi lake walikwisha jipatia kwa kupitia njia mbalimbali za udanganyifu zaidi ya shilingi bilioni 90 za kitanzania ambazo walizizungusha katika miradi mbalimbali. Tunafahamu kuwa baada ya jina lake kujulikana sana kuhusishwa na uanzishwaji wa Bank M Bw. Patel mapema mwaka huu alitaka kuuza hisa zake kwa Tarek Al-Asharam wa falme za kiarabu. Hatujui suala hilo liliishia wapi. Hata hivyo cha kutufanya tutake hili lichunguzwe ni jinsi gani Bank M iliwapima wawekezaji wake na kwa jinsi gani wawekezaji hao waliweza kupata jengo kutoka kwa aliyekuwa Rais bila kupimwa (vetting) kikamilifu na vyombo vya usalama. Jina la Bw. Jeetu siyo geni katika medani za makundi ya kihalifu nchini. Tunapozungumzia kuhusu kuwekeza katika fedha tunazungumzia jambo nyeti na la muhimu kwa taifa lolote lile. Leo hii tunashuhudia nchi za kimagharibi na zile nyingine zilizoendelea zinapojikuta katika hali tete ya kiuchumi kutokana na baadhi ya watu kukosa uaminifu katika sekta ya fedha. Leo hii katika Taifa letu sekta yetu ya fedha imefanyiwa michezo

ya ajabu na bado serikali yetu haijaitikisa vizuri. Watu kama kina Madoff wa Marekani ambao leo hii wameshtakiwa kwa kusababisha upotevu/wizi wa zaidi ya dola bilioni 50 kwa kile ambacho tungeweza kukiita ni “uwekezaji”!

safari hii akijifanya ni mwekezaji. Kwa kutumia fedha za ambazo chanzo chake ni cha mashaka akaanza “kuwekeza” kwenye makampuni mbalimbali halali na hivyo kuanza kuchuma fedha “halali” kwa kutumia mtaji usio halali.

Jeetu Patel ni mhalifu wa kimataifa ambaye anajulikana hivyo. Ameshahusishwa na kesi mbalimbali za wizi wa kutumia makampuni ya uongo na pia inadaiwa amewahi kuhusishwa na kukamatwa kwa kontena la madawa ya kulevyahaya mapema Magazeti miaka ya 90. Inashangaza jinsi gani mtu huyo huyo anaweza kuingia katika yanahaririwa nasekta ya fedha nchini!

Ni mdau wa Jeetu kwenye makampuni hayo mengine hapo juu. Lakini huyu anatushtua zaidi kwa sababu ya uhusiano wake na Benki Kuu. Amemuoa binti ya Sukhi Shah aliyekuwa mbunifu wa majengo ya “Minara Pacha” ya Benki Kuu. Akiongoza shirika la mkwe wake alifanikiwa kupata mradi huo wa kusanifu majengo hayo ambayo inadaiwa yanaweza kuingia kwenye vitabu vya rekodi za dunia vya Guiness. Majengo hayo kama yangejengwa kwenye Jiji la New York (miongoni mwa miji iliyo ghali sana duniani) yangegharimu kama dola milioni 75. Hata hivyo majengo hayo bado yanaendelea kujengwa kwa zaidi ya Bilioni 350 za Kitanzania! Licha ya kilio cha wabunge na watu mbalimbali bado hatua thabiti za kufuatilia hazijafanyika. Kinachotushtua zaidi ni ule uwezekano wa mtu ambaye ameshawahi “kukuchapa” kwenye nyumba yako unampa nafasi ya kukubunia nyumba nyingine! Je akiweka milango ya siri itakuwaje?

wahariri wale wale

Ni kwa sababu hiyo tunaona ni lazima kuchunguza makampuni yote ambayo Bw. Jeetu Patel anaonekana jina lake. Miongoni mwao ni pamoja na Noble Azania Group of Companies, B & V Holdings, V&B Asso-

ciates, Bora Apartments, Noble Motors, na mengine mengi ambayo tuna uhakika serikali inayafahamu. Tunachodai ni kuwa Bw. Patel na washirika wake walitumia mbinu za kihalifu kujichotea mabilioni ya shilingi za Watanzania, wakazigeuza kuwa mtaji wa biashara zao na wakarudi kutumia biashara hizo “halali” kujipatia fedha zaidi kwa watanzania kwa kuwauizia huduma na bidhaa mbalimbali. Tunaamini mwizi ni mwizi hata akigeuka na kukiuza kile alichoiba kwenye soko la halali tena kwa watu aliowabia! Vimal Mehta Huyu ni mdau mwingine wa Benki M ambaye naye anauhusiano wa karibu na Jeetu Patel. Bw. Mehta anaonekana kwenye makampuni kadhaa ambayo Jeetu naye anaonekana na tunaamini kuwa kutokana na historia yake kinachowaunganisha ni uhalifu. Aliwahi kushtakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi katikati ya miaka ya tisini kuhusiana na uingizaji wa bia ya Stella Artois. Katika mazingira yasiyoeleweka kesi yake ilimalizika kimya kimya hasa baada ya yeye kutoweka nchini. Alirudi mwaka 2000 na

Kwa miaka ya karibuni amekuwa akijiweka katika mazingira ya kukubalika katika jamii kwa uwekezaji wake kwenye kiwanda cha bia cha Serengeti na michango yake mbalimbali kama alivyochangia dola 24,750 kwenye safari ya wagonjwa wa moyo waliopelekwa India mwaka 2006. Uchunguzi wetu unaonesha kuwa Bw. Mehta anaonekana tena katika kampuni ya Merlin International ya kigogo mwingine wa uchotaji wa fedha za umma Tanil Somaiya ambaye ni mshirika wa karibu wa mtuhumiwa wa ununuzi wa rada ya kijeshi ambaye anachunguzwa na Uingereza Bw. Shaileth Vithlani. Inaonekana kama vile kuna “kakikundi” ka watu wale wale ambao wamekuwa wakitumia ujanja wao kujichotea mabilioni ya fedha kwa wizi, kuzizingusha katika biashara halali na hivyo kujifanya kuwa ni wafanyabiashara halali. (Inaendelea wiki ijayo)

KARIBU MWANAKIJIJI.COM

JUZUU 5, TOLEO 19

PAGE 3

HOJA YA NGUVU KESI DHIDI YA MKAPA Na. Rev. Kishoka Jinsi kila kitu kinavyosambaratika na kuangamia, uharamia, uzembe, ukosefu uadilifu, kukosa uungwana na utu, hujuma, wizi, ufisadi na dhuluma zikiongezeka, vidole vyote vinabidi vimnyokee mtu mmoja, Benjamin William Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndiyo, Mchungaji kanena msilishangae. Ndiyo, Mchungaji kanena pamoja na kumshikia bango Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuwa mgumu kufanya maamuzi mazito kuisafisha nchi yetu, lakini badala ya kuendelea kumwagia Kikwete lawama, Mchungaji anasema, turudi kwa yule aliyekuwa madarakani kabla ya Kikwete. Wengine wenu mtadai turudi nyuma kwa Mzeee Mwinyi hata kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mimi nasema hapana, tunaanzia na Mkapa wala si kulitafakari Azimio la Zanzibar bali ni utendaji kazi wa Serikali ya Mkapa na uongozi wake Serikalini, Chama cha Mapinduzi na Taifa zima. Nilipoandika mada kuhusu Andrew, Omari, Cornell na Robert, niliwataja wakuu wa mambo ya sheria na dola, usalama wa Taifa na nchi, katiba na haki na kuwatuhumu kuwa wao katika nyadhifa zao na wakati wa uongozi wao, Tanzania iligeuka kuwa dangulo na handaki la kila aina ya uharamia kuliibia Taifa wazi wazi bila woga wala aibu. Kikwete katuambia, tumuache "Mzee Mkapa" astaafu kwa amani, mimi nasema hapana, hatuwezi kuendelea mbele bila Mkapa kufikishwa kizimbani na kujibu mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, kushindwa kulilinda Taifa kutoka maadui na uhalifu na mbaya zaidi kuliingizia Taifa hasara. Simtuhumu Mkapa kwa wizi, bali nalisema wazi kuwa ndani ya utawala wa Mkapa wa miaka 10, makovu na majeraha tunayoyaona leo hii ya uhujumu na ufisadi, yalianzia nyakati hizo, michubuko na mikwaruzo ilifanyika nyakati hizo na tulichobakishiwa ni uozo ambao

unatambaa kama algae na fungi. • Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.



Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.



Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.



Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato.



Sheria na Katiba: kuendelea kuwepo kwa sheria na mambo mabovu katika sheria na katiba ambayo yameondoa kabisa mihimili ya Bunge na Mahakama kuwa na nguvu za kikatiba na mamlaka kuihakiki Serikali kuu.



Uchumi wa nchi, kudorora kwa uchumi kwa hali halisi ya uzalishaji mali, kudumaa kwa kilimo na kukimbilia utegemezi wa kuagiza chakula, kupungua uzalishaji mali kutokana na kosekana kwa umeme, maji, barabara nzuri.



Elimu na Afya: kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania kwa kuruhusu matakwa binafsi ya watu wachache waamue kubadili mfumo wa Elimu bila kupata ushauri wa wataalamu wa Elimu. Afya kuendelea kudorora huku kukiwa na uhaba mkubwawa vifaa, madawa na wataalamu wa afya. Pamoja na yale machache tuliyoyashuhudia ambayo tunayaona kuwa ni chanya, kama kufutiwa madeni yetu na harakati za kuendeleza Mkukuta na Mkurubita, lakini ukweli wa mambo unabakia kuwa kama kweli Mkapa aliacha misingi imara, basi pamoja na Kikwete kujenga baraka la mawaziri kubwa na la kifahari, uchumi na pato la Taifa lisinge-

poromoka jinsi lilivyoporomoka kwa haraka. Ni wajibu wetu wote kama taifa kuwajibika na kuchapa kazi ili kulikwamua Taifa kiuchumi ili kuwepo na elimu na afya bora, ajira na tumaini la kuwa Taifa linalojitegema, lakini kinara, kiranja mkuu ambaye alitutukana kuwa tuna wivu wa kike na ni wavivu, matusi na lawama za Taifa kushindwa kusonga mbele zinarudi kwake na si mtu mwingine. Ni haki yetu kama Wananchi, kutaka Mkapa awajibishwe kwa kuvurunda kazi. Hata pamoja na kuwa hawezi kupigiwa kura tena, lakini anapaswa afikishwe mahakamani kwa uzembe na matumizi mabaya ya madaraka yake. Suala la Kinga ni la kitoto na linaendelea kulea uozo, ujuvi na ubabe wa kutishana na kulindana. Atakapofikishwa Mkapa mahakamani, hata kina Rostam, Lowassa, Chenge na wengine watabaini kuwa Watanzania, hatutaki mchezo. Kila mwenye ndoto ya Ufisadi, Uzembe, utumiaji vibaya madaraka, uvivu na kukosa kuwajibika ama itabidi atafute nchi nyingine ahamie au anyooke na kuanza kuishi kama Mtanzania Mzalendo. Kura zile za Tsunami hazikuwa za kutuletea Ze Comedy! Bwana Kikwete nakuomba fanya kazi yako, ondoa magugu, visiki na viwavi jeshi walio ndani ya Serikali na Chama chako. Jaruzelski, pamoja na yote aliyofanya kwa madai ya kutumia madaraka au kwa mujibu wa sheria, leo hii yuko mahakamani kujibu mashitaka. Kila kona dunia hii, kiongozi aliyebainika alifanya kosa anavuliwa kinga na kufikishwa mahakamani, kama rafiki yetu Chiluba alivyofanyiwa. Hivyo basi, tupaze sauti zetu kwa nguvu tukimtaka Kikwete amfunge paka kengele. Tunamtaka Mkapa.

Soma bure

MOTO WA MABADILIKO UMEANZA...

Picha ya Wiki

KATUNI ZA WIKI

Nairobi: Rais Kikwete alipotunukiwa Udaktari wa heshima

JIUNGE NA WANAKIJIJI WENZAKO!

http://www.mwanakijiji.com Jiandikishe kushiriki mijadala, kupata habari, kusikiliza muziki masaa 24 na matangazo ya moja kwa moja kila mwishoni mwa juma. Ukizungumzia habari, unatuzungumzia sisi!

K ut oka

kw enye

m tand ao

Mimi naamini Mkapa ndiye aliyeweka misingi ya Ufisadi katika nchi yetu founder of grand corruption in this country) na pamoja na hayo uliyosema, mengineyo ni:-

Huu ni upumbavu, yaani kweli ktk watz Cheche za Fikra milion 35 na ushee kweli hakuna wale Mchapishaji na Mhariri Mtendaji wenye uwezo wa kufanya kazi na ikaonekana au ndio kila anaepewa madaraka anataka kwanza kujifisadia yeye na familia M. M. Mwanakijiji yake. Lakini ndio matunda ya Rais kucha1. Kujimilikisha mgodi wa Makaa ya gua wakurugenzi wakuu wa mashirika ya Timu ya Waandishi Mawe Kiwira umma, inatakiwa watu watangaziwe ajira Benjamin Mwalukasa— Mhariri 2. Kufanya biashara akiwa Ikulu na ya ukurugenzi then kila mtu apeleke CV kuondoa utakatifu wa Ikulu yake pale na wakati wa mahojiano Freddy Katunzi—Habari za Siasa 3. Kushindwa kuteleza makubalianao ya atatueleza nini kakusudia kulifanyia shirika mwafaka wa Zanziba waliyotia saini tajwa—Mjuba wao wenyewe.—Ibra Mahmoud Rashid—Habari mbalimbali Kubatilisha uamuzi wa kununua hayo maTunakokwenda itafikia wakati kutajenereta hakutoshi, waziri anatakiwa kuwaJessica L. Fundi – Makala kuwa na tume ya kuichunguza tume jibika au kuwajibishwa, ajiuzuru, kwani fulani kama kweli ilifanya kazi yake viameonyesha udhaifu mkubwa wa uelewa Kwa kujiandikisha, zuri!Kama mambo yenyewe ni hivi basi wa mambo yanayohusu sheria na taratibu maoni, habari, na ushauri tufute wizara na taasisi za umma na za nchi. Hivi waziri mzima hajui kwamba ni badala yake ziongozwe na TUME! makosa kisheria kwa serikali kununua miTuandikie: [email protected] Viongozi wetu tulionao sio viongozi wa tumba? Pia hajui kwamba kuna azimio la Wananchi ni viongozi wa matumbo yao bunge linalokataza biashara yoyote kati ya na familia zao.MUNGU IBARIKI TANZA- serikali na Richmond/Dowans– Mkoloni Tovuti: http://www.mwanakijiji.com NIA—Advocate Jasha Feleshi, andaa kesi kwa hawa mafisadi wa ATCL. Huu ni wakati wakusafisha sekta zote za serikali—Kasuku

CHAPA NA MPATIE MTU MWINGINE BURE

Kanusho: Mawazo yanayonukuliwa hayawakilishi msimamo au mawazo ya mchapishaji na utawala wa kijarida hiki.

Related Documents


More Documents from "Subi"