M O T O WA MA BA DI L I K O UM E ANZ A . . .
Cheche za Fikra
J U ZU U 7 TO LE O 27 FEBR UAR I 1 1 , 2 0 08
KIJARIDA CHA BURE— UKISHASOMA MPE MWINGINE—USIBANIE!
WIZI WA MABILIONI BOT
YA MALEGESI KAMA YA BALALI? wizi wa EPA kinaelekea kwingine. Hadithi mpya inaanza kutungwa baada ya mmoja wa watuhumiwa wakuu wa wizi wa mabilioni ya Fedha kutajwa kwamba ni mgonjwa katika hospitali ya Mikocheni kwa karibu siku kumi sasa.
Mdau wa Benki M—Mhe. Nimrod E. Mkono
Na. Fred Katunzi
Siku mbili baada ya kijarida chako ukipendacho kuripoti kuhusu sakata la Kagoda na yakuwa siyo gumu kulishughulikia kuna habari kuwa mmoja wa wahusika wakubwa wa sataka la EPA
ni mgonjwa na harakati zinafanyika ili kumpeleka nje kwa “matibabu zaidi”. Dalili zote hata hivyo zinaonesha kuwa kisa cha uchunguzi wa
Habari nyingine zinasema ameshatolewa hospitali akiwa anasubiri pasi yake ili aweze kwenda nje lakini habari nyingine nazo zinadokezwa kuwa “bado” yupo hospitali. Bw. Bered Malegesi ambaye kijarida Akiondoka huyo nchini chako kiliandika habari zake stori ndiyo imekwisha! kwenye toleo letu la tarehe 24 Januari, 2009 amelazwa hospitali hiyo kwa takri-
HOJA YA MWANAKIJIJI — BUNGE LISIITISHIE MAHAKAMA! Kuna msemo unasema kuwa “mgema ukimsifia tembo hulitia maji”. Kauli za vitisho dhidi ya Mahakama ambazo zimetolewa na Spika wa Jamhuri ya Muungano kwa kile kinachoaminika kuwa ni kumjibu Jaji Mkuu ni kauli za kusikitisha. Kati yetu tuliofurahishwa na jinsi wabunge wetu wame-
kuwa wakiisimamia serikali hatukutarajia kuwa Bunge hilo hilo litaanza kudai “supremacy” juu ya mihimili mingine ya Dola. Hili halikubaliki. Mahakama zetu hazitakiwa kuwa chini ya utisho wa Rais au Bunge kwani vyote ni vyombo sawa vyenye majukumu tofauti kabisa na
vikitimiza wajibu wake vinategemeana. Spika Sitta asifikiri hata kidogo kuwa Bunge analoongoza liko juu ya Mahakama. Haliko na haliwezi kuwa. Vinginevyo tutataka majaji na mahakimu wote wagome hadi Spika afute vitisho vyake.
Benjamin. G. Mwalukasa
Kijarida Ulichoshika • Kinatoka kila Jumanne • Ni cha bure kabisa! • Kisichofungamana na chama chochote au fisadi yeyote! • Kiko huru, kinathubutu, na hakiogopi mtu au hoja yoyote. • Ni kijarida chako! • Haki zote za kuchapa na kunakili zimeruhusiwa!
Ndani ya Toleo Hili Ya Malegesi na Balali
1, 2
Hoja ya Mwanakijiji
1
Chenge muda tu!
2
Masha alificha nini?
3
DaJessy: Mkuchika wapi?
3
Maoni ya Mtandao
4
Picha na Katuni
4
PAGE 2
CHECHE ZA FIKRA
YA MALEGESI KUWA KAMA YA BALALI? bani siku kumi sasa. Gazeti la Nipashe liliripoti kuwa Bw. Malegesi ameshauriwa na madaktari wake kusafiri kwenda nje kwa matibabu. Na jambo hili ndiyo linatushtua sisi kwani mazingira ambayo yameanza kutengenezwa sasa ni kama yale ya kuondoka kwa Gavana Balali kwenda ng’ambo kwa matibabu ya kile ambacho tuliaminishwa kuwa ni sumu. Kufanana kwa matukio haya kunatufanya tuhoji kwa kiasi kikubwa jitihada zozote za kupata ukweli kutoka kwa Bw. Malegesi ambaye ukiondoa marehemu Gavana Balali anabakia kuwa mtu muhimu zaidi katika kesi za EPA na hasa katika kupata kiini cha sakata la kufunua wahusika wakuu wa Kampuni ya Kagoda Agriculture ambayo inatuhumiwa kuchota karibi Sh bilioni 40. Katika toleo letu hilo tuliandika hivi kuhusu Bw. Malegesi “Mtu wa tatu ambaye ni muhimu katika kuijua Kagoda ni Mwanasheria Beredy Sospeter Maregesi. Mtu huyu ni muhimu kwanza kwa sababu iliyowazi kwamba jina lake linatajwa katika makampuni mawili ambayo yanatuhumiwa kuchota fedha za EPA. Makampuni hayo ni Malegesi Law Chambers na G&T International Ltd. Kwanini hadi sasa Bw. Meregesi hayafikishwa mahakamani? Jibu lake tunaamini liko kwenye sababu ya pili kwanini tunaamini mtu ambaye licha ya
kushtakiwa kwa makosa yake yeye mwenyewe lakini pia anashikilia ufunguo wa kumwelewa ni nani aliyechukua fedha Benki kuu.” Tuliandika pia kuwa “Kwa mujibu wa vyanzo hivyo Bw. Peter Noni na Malegesi ni miongoni mwa watu wachache wanaojua ni nani hasa waliochukua fedha za EPA kwa kutumia kampuni ya Kagoda.” Hivyo habari kuwa Bw. Malegesi ni mgonjwa na ya kuwa anahitaji matibabu nje ya nchi zinatufanya tuamini kuwahaya kuna kitu Magazeti kinasukwa. Kwanza, tunahoji tulichohoji kuwa ni kwanini Bw. Maregesi ha-na yanahaririwa jafikishwa kizimbani hadi hivi sasa?
wahariri wale wale
Yawezekana kuna sababu za uchunguzi lakini uwezekano mkubwa ni wa yeye naye kutoweka nchini kwa kisingizio ambacho ni vigumu kukipinga. Kile cha ugonjwa kama ilivyokuwa kwa Gav. Ballali. Kama vile ilivyotokea kwa Balali kuna uwezekano kuwa Bw. Malegesi naye akajikuta anaenda kwa matibabu ya muda mrefu huko ng’ambo endapo ombi lake la kusafiri litakubaliwa. Katika kisa cha Gav. Balali inakumbukwa jinsi ambavyo malegesi vyetu vya habari vilijazwa habari ya ugonjwa hadi hatimaye kifo na mazishi yake huko Marekani kitu ambacho kinaaminika ndicho kilichofungua uwezekano wa kesi za EPA kuendelea kwani shahidi muhimu hayupo tena. Baada ya toleo letu la tarehe 24 ambamo
Ni masaa au siku chache zimebakia kabla ya aliyekuwa Waziri wa Miundo Mbinu katika serikali ya Rais Kikwete na pia Mwanasheria Mkuu wakati wa Rais Benjamin Mkapa kufikishwa mahakamani katika kesi ambayo inatarajiwa kuvuta hisia na usikivu wa watu wengi ya ununuzi wa Rada ya Kijeshi yenye matumizi ya kiraia pia. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu Bw. Andrew Chenge pamona na wahusika wengine tuliowataja huko nyuma anatarajiwa kufikishwa kizimbani kujibu mashtaka mbalimbali ikiwemo ya kutumia madaraka kulisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi hasa baada ya kugundulika
Mojawapo ya vyanzo vyetu vya uhakika ameiambia Cheche kuwa kinachogomba hadi hivi sasa ni jinsi gani ya kumshughulikia Bw. Malegesi. “Unajua yeye ni mwanasheria na kuanzia mwanzo alikuwa amejitengenezea mazingira ya nini afanye mambo yakiharibika” amesema afisa mmoja mwenye ujuzi wa sakata hili jipya. “ Kitu ambacho ni kigumu sana kwa waendesha mashtaka na watu wengine ni kuwa Maregesi hawezi kusimama kama alivyo akiwa mshtakiwa” amesema ofisa huyo ambaye aliomba kutokutajwa jina wala ofisi yake. Kwa mujibu wa afisa huyo watanzania wasije kushangaa wakiona Maregesi akipanda kizimbani kama shahidi wa upande wa mshtaka kama walivyomfanyia Noni (mtu mwingine ambaye anajua sakata la Kagoda na EPA kwa undani).
Hata hivyo kwa mujibu wa afisa wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ambaye naye aliomba kutotajwa jina lake kutokana na unyeti wa mipango yao nay a kuwa yeye si msemaji wa ofisi hiyo “lolote lile liwalo Maregesi atapanda kizimbani siku si nykuwa fedha zilizolipwa kama sehemu ya rushwa kupitia Shaileth Vithlani hazitorudi ingi” Hata hivyo afisa huyo anasema kuwa kitu pekee ambachohawataki tena. kuona ni Malegesi kwenda nje ya nchi Zaidi ya mashtaka hayo Bw. Chenge ana- kwa sababu yeyote ile. tarajiwa kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kuvunja sheria ya maadili ya vion- “Akiondoka hapa basi stori ndiyo imeisha harudi” alisema afisa huyo katika hali ya gozi kwa kutokutangaza mali yake kwa kukata tamaa. “Kitu anachoweza kufanya Kamishna wa Maadili. na sitoshangaa akifanya ni kwenda kudai pasipoti yake kutoka kwa kina Mwanyika Kwa vile ushahidi ni mkubwa mno wa mashtaka ya rushwa Bw. Chenge pamoja au kuwalazimisha wamshtaki badala ya kumzuia kuendelea na shughuli zake” na Dr. Idris Rashid na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Bw. Vincent Mrisho alisema ofisa huyo. wanaweza pia kushtakiwa kwa mashtaka ya rushwa chini ya sheria mpya ya TAKUKURU ambayo ina makosa mengi zaidi KARIBU MWANAKIJIJI.COM kuliko ile ya nyuma.
CHENGE KIZIMBANI—MUDA WAANZA KUHESABIWA Na. Mwandishi Wetu
tulielezea kuwa Bw. Malegesi ni miongoni mwa watu wachache kabisa wanaojua usia wa Balali na ambao wamepata nafasi ya kuona/kuhifadhi nyaraka zenye ushahidi wa Kagoda basi ni wazi kuwa Bw. Maregesi ni “target” aidha ya wahusika wengine wa EPA au ya watu ambao wanaamini kuwa ni muhimu kufanya liwezekanalo kumnyamazisha au kuhakikisha kuwa hatopata kamwe nafasi ya kusimama kwenye kizimba aidha kama mshtakiwa.
JUZUU 7, TOLEO 26
Na. R Chasemwa
PAGE 3
HOJA YA NGUVU MASHA KUNA KITU ALIFICHA!
Mh Waziri ameonyesha uwezo katika kujielezea na kujenga hoja, barua yake imedhihirisha hivyo. Anaelezea, tuliona tender isiwe restricted na iwe wazi ilikuondoa hisia kwamba zabuni hii ilimlenga mtu au kampuni fulani, hatuambiwi ni kikao au chombo kipi cha serikali kilitoa mapendekezo hayo.
7% kati ya makampuni 104 yaliyovutiwa na tender ndiyo yaliyo fikia viwango vya tender.
Hii ni dhahiri kabisa kuwa wataalamu wa bodi waliliona hili tangu awali kwa ujuzi na uzoefu wao, kuwa kwenye mradi kama huu ambao unahusisha teknologia kubwa na ya kisasa ni vigumu sana kupata utitiri wa makampuni yanayofanya biashara ya taaluma Serikali isiyo sikiliza na kuwa heshimu wa- hii so ristricted tender ndio ilikuwa jibu. Hawa wataalamu ni wazalendo kuliko taalamu wa bodi ya wizara itakuwa na walakini. Kwa maelezo haya ni kuwa wa- hao wa upande mwingine kwa kulenga kuipunguzia serikali gharama za mchataalamu wa bodi walitaka tenda iwe restricted, na kusema kweli watakuwa wali- kato wa tender hii. tumia simple logic, nayo ni tenda ya wazi. Kampuni moja kati ya 46 zilizo ondolewa kwenye mchakato ndio waziri anasema Tenda ya wazi ikayavutia makampuni 104 (kielelezo A), Yaliyoweza kuwakilisha alipata malalamiko yake. Hii inatosha maombi 54, mchujo wa kwanza yakabaki kweli kumfanya mtu awaite watu Dodoma, kuwapa maelekezo kuangalia 21, yaliyo kuwa shortlisted 8 tu, kutoka mchakato, kutafuta ushauri PPRT n.Kk? 54 mpaka 8 yaliyo shindwa 46. Tujenge hoja kwa kutumia takwimu hizi:
hapana hapa kuna sababu nyingine imejificha haiingii akilini. Katibu mkuu kiongozi kumzunguka: Waziri ana kiri kuwa CS anauwezo wa kimamlaka na madaraka(kisheria) ktk utendaji wake kufanya alicho kifanya. Tujiulize huyu angekuwa anania hiyo angeagiza taarifa iletwe kwenye kikao cha baraza la mawaziri ambacho waziri ni mjube? nani kamzunguka mwenza kama tunataka kuwa wa kweli, Waziri aliyeandika barua ambayo hakumpa nakala CS au CS aliyekuwa akitekeleza wajibu wake? Hapa tunaona kuwa ni ubabaishaji tu unaoendelea. Hitimisho: Waziri kaingilia mchakato wa kumpata mzabuni kwa kutaka kuwabeba SAGEM SECURITE. Ajiwabishe kwa kujiuzulu. Asipofanya hivyo mamlaka husika imwajibishe kwa kumfukuza kazi. Wenye mamalaka wasipofanya hivyo basi tutashawishika kuamini kuwa pamoja na waziri, wao pia wanamaslahi binafsi.
DA’JESSY: KAPT. MKUCHIKA YUKO WAPI? Jessica L. Fundi Naomba nielezee masikitiko yangu juu ya utitiri wa magazeti yenye habari za uzushi, matusi ya wazi, na mapicha ambayo kama siyo ya kingono basi mpaka wake ni kijibandiko cha rangi nyeusi kuficha sura na sehemu za siri. Nasema nasikikika kwa sababu haya mambo ya viongozi wetu kukaa kimya hadi hali inakuwa mbaya sana tumeshayaona huko nyuma. Matatizo ya kifisadi ambayo yamekuwa yakiandikwa kwa miaka hii michache mengi yameanza na kukua baada ya waliotakiwa kuyadhibiti kufumba macho na kukaa kimya. Hili linatokea pia katika uandishi wa habari na magazeti yetu ambapo sasa kazi ya kumlea mtoto wa Kitanzania imekuwa ngumu kupita kiasi. Imekuwa ngumu kwa sababu watu wenye nguvu za fedha na nguvu za kisiasa ndiyo hao hao wenye kumiliki vyombo vya habari au wanauhusiano wa karibu na wamiliki hao kiasi kwamba hakuna tena mwenye kuthubutu kusema “hiki ni marufuku”.
Mpaka ambao unaonekana kuvukwa sasa ni malumbano kati ya wanasiasa na watu wengine wenye nguvu nchini, malumbano ambayo yamegeuza kurasa za magazeti yetu kuwa uwanja wa vita vyao. Watu hao ambao wana maslahi mbalimbali siyo tu wana lengo la kuharibiana wao wenyewe lakini kwa kiasi kikubwa wanashiriki kuaribu fikra changa za watoto wetu kwa kupandikiza mawazo yanayokaribiana na ya kishetani. Waandishi na wapiga picha za magazeti mbalimbali wanaandika habari kwa kuthubutu kuona kama kuna mtu yeyote anayeweza kuwanyoshea kidole huku wengine wakiandika hadithi na stori ambazo zina lengo la kuamsha ashki kwa anayezisoma. Ombi langu kwa Mhe. George Mkuchika na timu yake ni kuwa kama wanataka kuwa na biashara ya watu wa zima katika masuala ya kingono na mapicha ya ngono (pornography) basi serikali yake ije na sera itakayosimamia biashara hiyo kama inavyofanywa katika nchi nyingi za kigeni. Kwa kufanya hivyo watasababisha vyombo vya habari kufuata maadili na uandishi unaoendana kweli na wasomaji wao au walengwa wao na kuratibu biashara hiyo kisheria na kupata mapato ya kodi.
Vinginevyo sisi wazazi tunapojitahidi kulea watoto wetu katika maadili mema tusipewe uzito mwingine na serikali au uongozi ambao uko butu katika kutelekeza majukumu yake. Vinginevyo, mimi mwenyewe nimechoka na kupambana na nguvu kubwa namna hii wakati najaribu kulea watoto wangu. Kama Mkuchika hawezi kusimamia sheria ya magazeti au sheria nyingine na kama serikali imeshindwa kuhakikisha magazeti yanafuata sheria na maadili kulingana na wasomaji wao basi waseme ili na sisi wengine tuanze kufikiria jinsi ya kujichukulia sheria mikononi. Mhe. Waziri chonde baba amka!
[email protected]
Soma bure
MOTO WA MABADILIKO UMEANZA...
Picha ya Mwaka
KATUNI ZA WIKI
Waziri Masha na Dr. Slaa Bungeni wiki iliyopita!
JIUNGE NA WANAKIJIJI WENZAKO!
http://www.mwanakijiji.com Jiandikishe kushiriki mijadala, kupata habari, kusikiliza muziki masaa 24 na matangazo ya moja kwa moja kila mwishoni mwa juma. Ukizungumzia habari, unatuzungumzia sisi!
K ut oka
kw enye
m tand ao
Sitaki nikufundishe nini cha kufanya Dr.Slaa lakini moja tu,CHUNGA SANA! Usipende kukaa sehemu moja mara mbili au muda mrefu. Uwe kama Kinyonga katika nyendo zako. Wapo watakao kuwa wakikufuatilia sana kila uendako na kila ulifanyalo.– Kurutamatata
Mbona Mh. Waziri Masha hakuambatanisha barua kutoka SAGEM SECURITE ya udhibitisho wa malalamiko yao kwake juu ya kuridhishwa na mchakato wa uachambuaji wa zabuni?? Iweje Ofisi nyeti kama hiyo iendeshwe kwa habari za kupeana kwenye vilabu vya pombe au disco.— Bagaga
Hiki ni kitendo cha aibu kwa serikali yetu, kwa nini juhudi kama hizi za kupata habari zisifanywe ili kuokoa maisha ya albino na kufichua wahujumu uchumi (Mafisadi) ambao wanakaa vikao vya siri na kupanga madili ya kuwaibia watanzania? - Hoftsede
Ila nimewasifu mashushushu walioko kule Geneva wametusaidia kujua haya. Ila Jk hawezi kumuondoa jamaa ni swahiba wake na si unajua toka kwenye kampuni ya uwakili ya kina masha na wenzake jk ameshawatoa karibia wote, kuna mmoja majuzi juzi kachaguliwa kuwa Jaji.—Mjub
Hili la kuomba ulinzi litakuwa na maana kama waliowatega sio hawo watakao ombwa ulinzi. Kama ikibainika waombwa ulinzi ndio walio watenga sasa siwatakuwa wamewarahisishia kazi. Jamani tuwe wangalifu na makini tunapotoa ushauri au ndio nyie walewale maana mnambinu nyingi za kuwamaliza watu ikishindwa hii mnaingia na nyigine papohapo. Longii Twiga
Barua zimepindishwa si kwa nia njema ya ama kumrekebisha Mh Masha, bali ni kumdhalilisha—Dickabudi
Cheche za Fikra
Mchapishaji na Mhariri Mtendaji M. M. Mwanakijiji Timu ya Waandishi Benjamin Mwalukasa— Mhariri Freddy Katunzi—Habari za Siasa Mahmoud Rashid—Habari mbalimbali Jessica L. Fundi – Makala Kwa kujiandikisha, maoni, habari, na ushauri Tuandikie:
[email protected] Tovuti: http://www.mwanakijiji.com Kanusho: Mawazo yanayonukuliwa hayawakilishi msimamo au mawazo ya mchapishaji na utawala wa kijarida hiki.