Futurist Manifesto

  • May 2020
  • PDF

This document was uploaded by user and they confirmed that they have the permission to share it. If you are author or own the copyright of this book, please report to us by using this DMCA report form. Report DMCA


Overview

Download & View Futurist Manifesto as PDF for free.

More details

  • Words: 2,183
  • Pages: 7
FUTURIST MANIFESTO Tumekuwa tukisimama usiku kucha, mimi na marafiki zangu chini ya taa za duara za shaba zimulikazo mioyo yetu kwa sababu nazo zilikuwa zimemulikwa kwa nguvu za mioyo ya umeme kwa kutetemeka kutokana na uvivu wetu wa asili, tukiwa kwenye madhuhulia ya kifahari ya kiuajemi, tukibishana na kuchorachora kwenye karatasi kama vichaa. Mioyo yetu ilijaa furaha isiyo kifani kwa kuwa tulijisikia tupo peke yetu kabisa kama minara ya taa za kuonyeshea meli, au askari wa dolia aelezekaye macho yake upande wa jeshi la maadui waliojifanyia kambi mbele yake. Tukiwa peke yetu, na waandishi tu, chini kabisa ya matanuri ya mikaa ya kuendeshea meli, na roho wabaya waliofanya mstari katikati ya kundi la vibaka, na walevi,waliokuwa wakitapatapa na kupapasa kuta. Mara tukakatishwa na sauti ya tramu za ngazi mbili zilizokuwa zinapita zikiwa zimepambwa kwa mistari ya mianga kama kijiji kifanyacho sherehe, ambazo mkuu wao wa marubani alikuwa katika mawimbi akianguka na kuinuka kutokana na mawimbi yaliyosababishwa na gharika, yakimkokota kuelekea baharini. Kisha kimya kikaongezeka! Tukiwa tunasikiliza sauti ya mfereji uliochakaa na kubomokana wa jumba bovubovu la kifahari na majani yaliyoota juu yake, mara magari matupu yalijisogeza chini ya madirisha yetu. Njooni rafiki zangu! Nikasema; twende zetu! Mwisho visasili na mafumbo ya wazo kuu vikawa vimesahaulika. Tutakuwepo atakapozaliwa Kenturo na mara tutawaona malaika wakiruka kwa mara ya kwanza. Lazima tuyavunje malango ya uzima, ili kuvijaribu vitasa vyake na komeo zake. Twende! Naona jua la adhuhuri kabisa likiangaza dunia. Hatuna cha kulinganisha na uzuri wa silaha yake nyekundu ambayo inalipiga kwa mara ya kwanza kabisa giza letu nene. Tukaziibukia mashine tatu zilizokuwa zinakoroma na kuyagusa matiti yao. Nikajilaza jirani na wangu, kama maiti iliyo kwenye jeneza, lakini ghafla nikaamka na kuwa macho chini ya usukani; kisu kikubwa kililishtua tumbo

langu. Wazimu mkubwa ukaturudisha katika hali yetu ya awali na kutuzungusha mitaani, mwinuko mkali na kina kirefu kama mvo uliokauka. Hapa na pale kulikuwa na mwanga kwa mbali kupitia madirisha uliotufanya tusiamini macho yetu. Harufu! Nilipiga kelele; harufu ni nzuri kwa wanyama pori. Na tukawinda kama wanasimba, kifo na manyoya yake meusi, chenye mabaka ya misalaba ya samawiati kikitukimbiza katika anga lililochafuka lakupapasika na linaloishi. Hata hivyo hatukuwa na bibi kizee wa uhakika aliyeweza kulitanua umbile lake hadi mawinguni wala malkia katili wa kumtolea miili yetu aliyejigeuza kuwa na umbile la kiajemi! Hakuan sababu kufa isipokuwa kwa lengo la kujitoa kutoka uzito mnene wa ushujaa wetu! Tuliendelea kuendesha tukigandamiza magurudumu yetu yaliyokuwa yanawaka na kung'aa kama rangi za shati ndani ya pasi huku mbwa wakiwa katika ngazi za nyumba. Kifo, kwa upole kilinitangulia katika pembe zake , kikininyoshea mkono kwa ukarimu wote, na wakati mwingine kililala chini kikitoa mlio wa mkwaruzo wa meno kikinichungulia kutoka chini ya vidimbwi. Tuache busara nyuma yetu na ganda baya kama punje ya tunda na kwa majivuno tujitupe ndani kabisa ya mdomo na kifua cha ulimwengu! Tuwape chakula watu tusiowajua, sio kwa sabababu ya kukata tamaa, bali kwa lengo la kulijaza ziwa la upuuzi lisilo na kina! Mara baada ya kumaliza kuyasema manemo haya niligeuzwa haraka katika njia yangu na wazimu wa manambwa waliokuwa wakipigapiga mikia yao, na mara wakatokea waendesha baiskeli wawili waliokabiliana nami , wakiyumbayumba mbele yangu kama vile wananichunguza, kumbe wana lengo tofauti. Kuyubayumba kwao kwa kijinga kukaizuia njia yangu. Kuchoka kwake! Pouah! Nikasimama kidogo na kisha kwa karaa nikajirusha –Vlan; kichwa juu ya nyayo katika shimo. Oh! Shimo la mama! Matope kibao, bonge la mfereji! Nikatumbukia kwenye uchafu ulioshikamana ambao ulinikumbusha unyama wa nesi wangu kutoka Sudani! Nilipoutoa mwili wangu, matope yakatapakaa na kutoa harufu mbaya. Nikahisi ncha kali ikiuchoma moyo wangu niliona kundi kubwa la wavuvi

na jango la waganga wa kienyeji wakishangaa maajabu haya. Kwa uangalifu mkubwa waliinua winchi ya chuma ili kuliopoa gari langu kama papa mkubwa aliyezama ardhini. Ilitoka taratibu, ikiacha magamba katika shimo kama vile kiti cha thamani cha kukalia na mazuria ya kifahari. Tulidhani imekufa kabisa, papa wangu mzuri…kumbe nililiamsha kwa kuligusa mara moja tu kwenye mkia wenye nguvu, akafufuka na kuanza kukimbia kwa mbio zote kadili ya uwezo wa pezi zake. Halafu nikaugeuza uso wangu uiojaa matope , mikwaruzo ya chuma , jasho lisilo na maana na anga la masinzi katika malalamiko ya wavuvi wenye msimamo mkali na waganya wa kienyeji waliokasirika, tukaimrisha nia yetu ya kwanau na agano kwa watu wote waishio duniani. LENGO LA KISASA! 1. Tunataka kuimba utamu wa hatari, tabia ya nguvu na fujo. 2. Mambo muhimu ya uandishi wetu yatakuwa ujasili, ushujaa na uasi. 3. Fasihi sasa ina lengo la kukuza upana wa mawazo, upeo wa hisia na usingizi. Tunataka kukuza mbio za uchokozi, kutopenda kulala na kutembea mara dufu, kurukia sehemu za hatari, kupigana makofi na ngumi. 4. Tunatangaza rasmi kuwa uzuri wa ulimwengu umetajirishwa kwa uzuri mpya. Uzuri wa mbio. Gari litembealo huku boneti yake ikiwa imepambwa kwa mipira kama majoka yatoayo pumzi ya kulipuka, gari liungurumalo likiasilia kukimbia kwa mwendo wa risasi ya bunduki linapendeza kuliko ushindi wa samotrase. 5. Tunataka kumwimbia mtu aliye chini ya taili , mhimili kamili unaoimega dunia wakati wenyewe unajirusha nje ya mzunguko wake. 6. Mshairi lazima ajipe muda wa kujipasha joto, muda wa mahaba na ubatilifu ili kuongeza shauku ya ari ya vitu vya kwanza. 7. Uzuri upo katika jitihada tu. Hakuna jambo kubwa lisilo na ukatili ndani yake. Ushairi lazima uwe kuamsha fujo kwa kutumia nguvu zisizojulikana, kuzilazimisha kumtolea heshima mwanadamu. 8. Tupo katika urasimu mkubwa wa kisayari. Kuna haja gani ya kurudi nyuma wakati tutalazimika kufungua milango ya ajabu ya yasiyowekzekana? Wakati na mahali vilikufa jana. Sasa tunaishi katika ukamilifu kwa sababu tumeuumba umilele, mwendo uliopo katika hali zetu.

9.

Tunataka kuitukuza vita iliyo tiba pekee ya ulimwengu -ujeshi, uzalendo, hisia za uharibifu, na za utawala huria, mawazo mazuri yanayoua na dharau kwa wanawake. 10. Tunataka kuvunja jumba la makumbusho na maktaba, hamu ya kupigana, haki za wanawake, nafasi zote za matumizi ya uwivu. 11. Tutaimba juu ya mkusanyiko mkubwa uliotikiswa na kazi , anasa na uasi. Rangi mbali mbali na tunzi za sauti nyingi za kimageuzi katika ukuu wa kisasa, tetemeko la usiku la silaha, sehemu ya kazi chini ya mionzi ya umeme: vituo vya reli vyenye njaa vinawameza nyoka wajivutao, viwanda vimeachwa na watu wao kwa sababu ya moshi wake uliotapakaa; milima na wanamazoezi warukao wameviringishwa hadi ng'ambo ya biashara halamu ya mito iwakayo jua, meli za starehe zinanusa mihimili, magari moshi yakipumua kwenye barabara za meli kama punda wa ajabu wa chuma wenye mipira mirefu kwa kujidhibiti na mruko wa kutirizika wa ndege ambazo mitambo yake inatoa sauti ya mpeperusho wa bendera na makofi ya kundi la watu wenye hamu na shauku ya kitu. Hapa ni Italia, ambako tunaonyesha fujo hii ya uharibifu, ambyo kwayo sisi hivi leo tunautambua usasa, kwa sababu tunataka kuitoa Italia toka uozo wa maprofesa wake, wataalamu wa elimu kale, viongozi wa watalii na sehemu za vitu vya kale. Italia imekuwa kwa muda mrefu soko kuu la vitu vichakavu. Tunataka kufuta maduka ya vitu vya kale ambayo yanafunikwa na makaburi yasiyohesabika. Maduka ya vitu vya kale, makaburi! Yanaonekana kabisa sambamba na sehemu mbaya mbaya za miili ambazo hazitambuani. Nyumba za kulala unamolala kwa kubanana, iwe kwa vile unaogopa au hujui. Ukali wa kubadilishana wa wachoraji na wachongaji ambao wanauana katika nyumba hizo hizo za maonyesho kwa kurushiana kamba na rangi. Hutembeleana mara moja mwaka kama vile mtu atembeleavyo makaburi ya wafu, mara moja kwa mwaka; hilo tungeruhusu. Tunaweza pia kufikiri kuweka maua mara moja kwa mwaka katika miguu ya Giokonda. Lakini kwa huzuni yetu, ushujaa wetu na hamu yetu ya kwenda makumbushoni kila siku, hilo hatulikubali! Unataka kuoza? Utapata nini katika picha za kale zaidi ya upotoshi uletao maumivu wa usanii, ukijaribu kuruka mipaka isiyopitika ambayo inazuia ufafanuzi kamili wa ndoto?

Kustaajabia picha ya zamani ni kuumwaga ufahamu wetu katika sanduku la kuzikia badala ya kuusukumia mbele ya mbubujiko mkubwa wa ubunifu na matendo. Unataka kupoteza sehemu kubwa ya nguvu zako za kustaajabia kwa vitu vya kale visivyo na umuhimu, vitu ambavyo vitakufanya uchoke, uishe na ukandamizwe? Kwa kweli kutembelea makumbusho, maktaba na mashule (makaburi ya nguvu zilizopotezwa bure, jehanamu ya ndoto zilizonyongwa, rekodi ya mawazo mibaya!) kwa wasanii ni kitu kinachodumisha ubabaishaji kwa watu wazima na kwa vijana walioelimika nikulewa vipaji na malengo yao. Kwa wanaokufa, kwa vilema, na kwa wafungwa inakubalika. Maajabu yaliyopita yanaweza kuwa kitulizo kwa vidonda vyao kwa sasa wakati baadaye inawakataa. Lakini kwetu sisi hiyo haipo, sisi ambao ni vijana wanaoishi, wa kisasa, na wenye nguvu. Waacheni wateketezaji waje na vidole vyao vilivyo safishwa! Hawa hapa! Washa moto kwenye makabati ya maktaba! Pindisha mifereji ili kujaza maji vyumba vya nyumba ya maonyesho. Yaache maturubai ya kifahali yaelee ufukoni! Chukua sululu na nyundo! Fukua misingi na mifereji ya miji. Mzee kabisa kati yetu hana miaka zaidi ya thelathini. Tunayo sio zaidi ya miaka kumi kumalizia kazi yetu! Tukifikisha miaka arobaini vijana na wengine wenye nguvu kuliko sisi watutupe kwenye shimo la takataka kama karatasi zisizohitajika. Watakuja kutugeuka kutoka mbali, wakirukaruka kwa kiimbo cha nyimbo zao za kwanza, wakidaka hewa kwa vidole vyao vya kuibia na kunusa katika milango ya mashule harufu nzuri ya roho zetu zilizooza ambazo zimeshawekwa kwenye mahandaki ya maktaba. Lakini sisi hatutakuwepo huko. Mwisho wa majira ya baridi watatuona ndani ya kina cha nchi katika kiota chenye uchungu cha kusikitisha, tukitoa mwangwi kwa sauti za mvua ya vuli, tukiwa tumejikunyata jirani ya ndege zetu zinauzoyumbayumba , tukiota moto wa kimaskini na vitabu vyetu vya kisasa vikiwa vinawaka kwa furaha chini ya vimulimuli vya picha zao vipaavyo. Watatuzunguka wakipumua kwa shida na kwa kukata tamaa, wakiuzishwa na ushujaa wetu usio kifani, watajirusha mbele ili kutuua kwa chuki yao

yote kwa sababu mioyo yao itakuwa imeleweshwa kwa upendo na kwa kutushangaa. Toka hapo haki yenye nguvu na afya itang'ara kwa mionzi ya macho yao. Kwa vile usanii unaweza kuwa tu kwa fujo, ukatili na kutokuwa na haki. Wazee kabisa kati yetu bado hawajafikisha miaka thelathini na bado hatujapoteza thamani ya nguvu, upendo, ushujaa na nia thabiti, ya kudumu, yenye utamu wote, bila kufikiri, kwa uwezo wetu wote, hadi tutakapopoteza pumzi. Tuangalie! Hatujapoteza bado pumzi yetu, mioyo yetu bado haijachoka. Kwa vile imesafishwa kwa moto, chuki na kuharakisha. Unashangaa? Kwa sababu hukumbuki kuwa mzima! Tukisimama juu ya kilele cha ulimwengu, tunazindua tena mashindano ya kwenda nyotani. Una upinzani wowote? Sawa! Najua ni wazi! Tunajua yale tu yanayothibitishwa kwa akili zetu za udanganyifu. Sisi ni jumla na mwendelezo wa mababu zetu! Ikisema ! pendine! Sawa! Shida iko wapi? Lakini hatutasikiliza. Inua kichwa. Tukiwa kwenye kilele cha ulimwengu, tunazindua tena mashindano yetu ya fidhuli ya kwenda mwezini. Tunawahi kwenye mazishi ya kejeli ya uzuri wa passeist, (mwanamahaba, mfanya ishara na mtunzi wa nyimbo) ambaye vitu vyake vya msingi vilikuwa kumbukukmbu, hamu ya nyumbani, ukungu wa hekaya zilizotungwa zamani za kale, mvutio wa ajabu wa zama za kale, mifananisho, kutokamilika, ushamba, upekee mwitu, ghasia za aina mbalimbali, hali ya utusi utusi, ulafi, kuchoka, alama za uchafu wa miaka na miaka, kuvunjikana kwa magofu, kusujudu radha ya uozo, kukosa rajua, kifua kikuu, kujiua, kupunguza maumivu, uzuri wa kukosea na kuabudu kifo. Uzuri mpya umezaliwa leo, fujo, utata mpya wa wepesi wa kuhisi, uzuri uliopita, na hayo yote mimi ninayaita utamu wa kijometria a wakimahesabu. Alama zake ni: usahaulifu, afya, matumaini, hamu, nguvu iliyodhibitiwa, mbio, mwanga, msukumo, mpango, utaratibu, utii, mbinu, kutamani miji mikubwa, kukosa raju kwa ukatili kunakotokana na tabia ya misuli na michezo, mawazo yasiyo na mategemezo, umwagikaji, ukimya na kufanya mengi kunakotokana na utalii, biashara na uandishi wa habari, mateso kwa ajili ya mafanikio, hali ya uangalifu kwa ajili ya kufanya kumbukumbu, shauku kubwa ya kuiga, utengano na muungano, njia ziingiazo kwa furaha

na mawazo yaliyotiwa mafuta, kugombania nguvu kama zinavyokutana katika njia ya ushindi. Akili yangu ya kisasa ilielewa uzuri huu kwa mara ya kwanza juu ya mlima wa kutisha. Mbio za meli, njia zake za moto kutoka urefu wa meli ya mabehewa manne, ndani ya kaubaridi kanakoashilia uwezekano wa vita, uimara wa namna yake wa mipango ulioshushwa na adimira na mara moja unabaki peke yako, mtu hayupo tena, yupo haja, bila uvumilivu na ugonjwa wa dhahabu na shaba. Vyote hivi viliwasha hamu ya hesabu na jiometria. Nilisikiliza maneno ya kwanzna ya muziki wa umeme ukimwagika kupitia vizibo vya minara ya bunduki isiyo kwenye mifuko yake ikiwa tayari kurushwa. Maeneo ya juu, lango kipandisho, moto, mkwepo wa ghafla, njia na mipenyo binafsi, mpigo, mmvunjiko, harufu ya mayai yaliyooza, gesi yenye sumu, kutu, amonia, nk Huu mchezo mpya umejaa maajabu ya kisasa nauzuri wa kijometria. Unatuvutia mara elfu ya saikolojia ya kibinadamu na mchanganyiko wa mipaka yake. Muda mwingine mikusanyiko ya kibinadamu, kupwa kwa nyuso na milio ya mikono inaweza kutufanya tuusikie mhemko wa kiaina. Kwao tungependelea muungano wa pekee, mashine zinazofanya kazi zilizojipanga na zenye hamu. Hakuna kilichokizuri kuliko kituo cha umeme kivumacho, kinachosikika, kinachoshikilia nguvu za haidrali za mlima wa nyaya na nguvu za umeme wa horizoni kubwa, uliounganishwa kwa marumaru na kukaziwa kwa nambari za siri na mashine za kuchanganyia. Paneli hizi ni mifano tu ya uandishi wa mashairi. Kwa walio wahi tunawafundishaji na kundi kubwa la wanasanaa ambao katika mageuzi yao, mapumziko namaneno ya misuli yao wanathibitisha ukamilifu wao wa gia za uhakika na uzuri wa kijiometria tunaokusudia kuupata katika ushairi kwa maneno na katika uhuru wote. Imetafsiriwa na Castor Mfugale

Related Documents

Futurist Manifesto
May 2020 27
Manifesto
May 2020 51
Manifesto
December 2019 75
Manifesto
April 2020 51
Manifesto
June 2020 28
Manifesto
June 2020 25