KATIBA YA UMOJA GROUP SPORTS CLUB 1.0
UTANGULIZI: Baada ya kutafakari kwa muda mrefu ndugu na marafiki wa karibu waliona ni vizuri waunde chama chao au kikundi ambacho kitaweza na kitakuwa na utaratibu wa kueleweka na wa kudumu katika kusaidiana wakati wa shida na raha. Vikao mbalimbali vya chama hiki vilivyofanyika kwenye tarehe 4/3/2001 na 18/3/2001 ambapo maamuzi ya kuundwa katiba ya chama yalipita. Hivyo basi katiba hii inatokana na wajumbe watano waliochaguliwa na kikao cha tarehe 18/3/2001 na kuunda katiba rasimu ambapo baadae ililetwa kwa wajumbe kujadiliwa na kupitishwa rasmi.
2.0
JINA LA CHAMA 2.1 2.2
3.0
Jina la chama litakuwa UMOJA GROUP SPORTS CLUB. Makao yake yatakuwa Dar-es-Salaam. MALENGO/MADHUMUNI YA CHAMA
3.1 3.2
Lengo ni usaidiana wakati shida na raha. Shida zinazotambuliwa na chama ni kama zifuatazo:-
3.3 4.0
Ugonjwa Kifo Gharama za elimu.
Raha zinazotambuliwa na chama ni, sherehe za kufunga mwaka na sherehe za harusi.
SHUGHULI ZA CHAMA Kusaidia na kukuza hali ya maisha kwa wanachama kijamii, kiuchumi, kiafya na kielimu. Ikiwezekana kupitia kwa wafadhili.
1
5.0
UANACHAMA 5.1
Kutakuwa na utaratibu wa kujiunga na chama ambao unakubalika kikatiba.
5.2
Mwanachama kamili ni yule ambaye atatimiza masharti yote ya uanachama kulingana na katiba.
5.3
Sifa za Mwanachama i) ii) iii) iv) v) vi) vii)
5.4
Awe na miaka 18 au zaidi Awe wa jinsia yeyote Awe na akili timamu (Sound mind) Awe mtu wa kujituma Awe Mtanzania Asiwe mtu aliyefungwa jela kwa zaidi ya miezi sita Awe mkazi wa Dar es Salaam.
Kukoma Uanachama Uanachama katika Umoja Group unakoma iwapo patakuwa na: i) ii) iii) iv) v)
6.0
Kifo cha Mwanachama Kujiuzulu kwa hiari Kupatwa na ugonjwa wa kichaa au uwendawazimu Kufukuzwa na chama Iwapo mwanachama atahama pamoja na familia yake kwenda nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
HAKI ZA MWANACHAMA Haki za Mwanachama ni kama zifuatazo:i) ii) iii) iv) v) vi)
Haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi Haki ya kulinda na kutetea katiba Haki ya kupiga kura katika kupitisha maamuzi ya chama kwenye vikao Haki ya kusikilizwa na kujitetea mbele ya vikao vya chama Haki ya kujitoa au kujiuzulu kutoka katika chama Haki ya kudai risiti/stakabadhi ya malipo yeyote atakayofanya kwa chama.
2
7.0
WAJIBU WA MWANACHAMA i) ii) iii) iv) v) vi) vii) viii) ix)
8.0
Kutoa michango ya chama kama katiba inavyosema Kuhudhuria vikao vyote vya chama Kulipa faini inapotakiwa kufanya hivyo Kutoa michango ya vifo Kuhani na kushiriki kwenye misiba Kufariji na kutembelea wagonjwa Kushiriki katika kufanikisha harusi Kulinda na kuheshimu Katiba Kushiriki katika harambee.
NJIA ZA KUPATA FEDHA ZA CHAMA i) ii) iii) iv) v) vi)
9.0
Michango ya kawaida kutoka kwa wanachama Ada ya kiingilio (Entry Fee) Ufadhili/Misaada kutoka sehemu mbalimbali Mikopo, n.k. Faini Miradi mbalimbali. MUUNDO WA CHAMA
i) ii) iii)
Mkutano Mkuu wa Chama Halmashauri Kuu ya Chama Kamati Kuu ya Chama
9.1
Mkutano Mkuu wa Chama Wanachama wote
9.2
Halmashauri Kuu ya Chama Kamati Kuu na wajumbe wawili (2) walioteuliwa na Mkutano Mkuu.
9.3
Kamati Kuu ya Chama Mwenyekiti Makamu wa Mwenyekiti Katibu Katibu Msaidizi Mweka Hazina Wajumbe wawili (2) walioteuliwa na Mkutano Mkuu.
3
10.0 VIONGOZI NA JINSI YA KUWACHAGUA 10.1 Viongozi watakuwa: Mwenyekiti Makamu Mwenyekiti Katibu Katibu Msaidizi Mweka Hazina Wajumbe wa Halmashauri kuu Wajumbe wa Kamati Kuu.
10.2 Viongozi wote hawa watachaguliwa na Mkutano Mkuu 10.3 Uchaguzi wa viongozi utafanyika kila baada ya mwaka mmoja 10.4 Kiongozi atadumu kwenye uongozi kwa vipindi vitatu tu. 11.0 AKAUNTI YA CHAMA 11.1 Fedha za chama zitahifadhiwa kwenye benki ambayo itachaguliwa na wanachama kwenye mkutano mkuu. 11.2 Watu wanaokubalika kuchukua fedha (Signatories) kwenye akaunti ya chama ni Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Mkutano Mkuu. Fedha zitatolewa benki kwa idhini ya Halmashauri Kuu ya chama. 11.3 Ukaguzi wa fedha/mahesabu ya chama utafanyika mara mbili kwa mwaka au kwa dharura kulingana na hali au matakwa ya wanachama. 11.4 Ukaguzi wa mahesabu utafanywa na wajumbe waliochaguliwa na Mkutano Mkuu na ikibidi Mkaguzi kutoka nje ya chama kulingana na matakwa ya wanachama na sheria za nchi.
4
12.0 SEAL (MUHURI WA CHAMA) Kutakuwa na Seal (Muhuri) wa chama na Katibu wa chama ndiye atakuwa mtunzaji (Custodian). 13.0 MIPAKA YA HUDUMA ZA CHAMA 13.1 Wanaostahili kuhudumiwa na chama ni:-
Mume mmoja halali Mke mmoja halali Baba na Mama (Wazazi) Watoto Halali (wa kuzaa)
14.0 MENGINEYO 14.1 Maamuzi yote ya chama kwenye vikao yataamuliwa kwa njia ya demokrasia ambapo kura ya siri itatumika katika kufikia maamuzi. 14.2 Iwapo kura zitalingana pande mbili basi Mwenyekiti atatumia kura moja ya ziada ambayo ni ya turufu ili kufikia maamuzi.
MWENYEKITI – JOHN NKANE……………………………………. KATIBU – DR. M. MWANKEMWA…………………………………. TAREHE………………………….
5