Matukio Muhimu Yatakayokuwepo Katikati Ya Juma La 70 La Danieli

  • July 2020
  • PDF

This document was uploaded by user and they confirmed that they have the permission to share it. If you are author or own the copyright of this book, please report to us by using this DMCA report form. Report DMCA


Overview

Download & View Matukio Muhimu Yatakayokuwepo Katikati Ya Juma La 70 La Danieli as PDF for free.

More details

  • Words: 747
  • Pages: 3
1

Matukio Muhimu Yatakayokuwepo Katikati ya Juma la 70 la Danieli 1.

Kwa muhtasari          

 

 2.

Shetani anatupwa chini duniani kutoka mbinguni, Ufun.12:12; Shetani anampa uwezo Mpinga Kristo, Ufun.13:12; 2Wathes.2:9; Ulinzi wa yeye azuiaye unaondolewa, 2Wathes.2:7; Dan.12:1; “mtu wa kuasi” anafunuliwa, 2Wathes.2:3; Chukizo la uharibifu linatendwa ndani ya hekalu, Math.24:15; Agano na Israeli linavunjika, Dan.9:24; Mpinga Kristo anajiinua mwenyewe juu ya wote, 2Wathes.2:4; Mpinga Kristo anadai kuabudiwa na ulimwengu wote, Ufun.13:34, 12, 14b-15; Kahaba wa Babeli anangamizwa, Ufun.13:3-4,8,12-15; 17:16; Injili ya milele na onyo kwa wale watakaoipokea chapa ya Mpinga Kristo linatolewa kwa ulimwengu na wajumbe malaika wa Mungu, Ufun.14:6,8-9; Mashahidi wawili wanaanza huduma yao, Ufun.11:1-14; Mateso ya Waisraeli waaminifu (yaani mwanamke) na kanisa la kweli (mabaki ya wazao wake ambao wanazishika amri za Mungu na kutunza ushuhuda wa Yesu) yanaanza, Dan.12:1; Math.24:20b, 22-23; na Ukengeufu mkuu unaanza, Math.24:9-12; 2Wathes.2:3. Kahaba wa Babeli

Kahaba wa Babeli ni viongozi wa mfumo wa dini ya uongo au mifumo iliyoanzia Babeli wa kumuabudu Mama (Malkia wa Mbingu na Mtoto), mfumo ambao Shetani ameutumia na atautumia tena kuwadanganya mataifa kuhusu Kristo (uzao wa kweli wa mwanamke, Mwa.3:15, katika jitihada yake ya kuwaangamiza wateule wa Mungu, Dan.11:39; Ufun.17:1-7,9,15,18. Huu ni ukahaba wa kiroho. Angalia pia mlango wa 18 wa kitabu cha Ufunuo wa Yohana. Israeli pia ilionywa kwa kumuabudu malkia wa mbingu, Yer.44:16-19, 24-28 na matokeo yake mabaya kwa wale ambao hawakutii:

2

 Mfumo huu wa dini ya uongo utakaa juu ya maji mengi, yaani juu ya watu wengi wengi, mataifa na lugha mbali mbali watakaotawaliwa kutoka upande mmoja wa dunia mpaka mwingine;  Mfumo huu wa dini ya uongo utakuwa na nyenzo ya kisiasa, maana Maandiko yanatuambia kwamba, “atawala juu yaw wafalme wa dunia”;  Mfumo huu wa dini ya uongo kwa nguvu zote utaupinga Ukristo wa Kibiblia, yaani utalewa na “damu ya watakatifu na mashahidi wa Yesu”; na  Mfumo huu wa dini ya uongo utawakilisha “mji mkuu, utawalao juu ya wafalme wa dunia”, Ufun.187:18; 18:10,18,19,21) Mfumo huu wa dini ya uongo kwa karne nyingi kwa ujanja kabisa umemuondoa “uzao wa mwanamke” (Kristo) na kuweka kumuabudu mama na mtoto au “Malkia wa Mbingu” kulikolaaniwa kwa nguvu zote na manabii wa kale, Yer.44:16-19; 24:28. Angalia pia Ufun.17:2,3,6. Mwanamke kahaba huyu amewatawala kwa miaka mingi wafalme wa dunia. Vivyo hivyo, katika siku za mwisho, uhusiano ule ule na ufalme wa mwisho wa mnyama wa Shetani, kwa kutumia umaarufu wake wa kimatatifa alioujenga hapo kale, atamsaidia Mpinga Kristo kukusanya muungano wa mataifa kumi ambao utakuja kutawala dunia, Ufun.17:12,13. 3.

Kipimo (test) kwa namna mbili

Mpinga Kristo, mnyama wa kwanza atafunuliwa kama mtu aliyekuwa amekufa na kurudia tena uzima katikati ya juma la 70, ambapo atajiinua mwenyewe katika hekalu la Yerusalemu lililojengwa tena, na kujitangaza kuwa yeye ni Mungu na kudai kuabudiwa na ulimwengu wote. Ndipo atakapoanzisha kipimo (jaribio) la namna mbili ili kuwatambua:  wale watakaomuabudu na  wale watakaokataa kumuabudu na kujitoa kikamilifu kwake. Kipimo hiki kitatekelezwa na “mwingine” au “mnyama wa pili” ambaye ndiye mkaziaji mkuu wa maagizo ya Mpinga Kristo na “anatumia mamlaka yote ya mnyama wa kwanza”, Ufun.13:12.

3

Kipimo hiki kitakuwa na mambo mawili maalumu:  Kwanza, kila mtu atatakiwa “kuiabudu sanamu ya mnyama au kuuawa, Ufun.13:15; na  Pili kila mtu atatakiwa kuipokea chapa ya mnyama ama sivyo hawataweza kununua wala kuuza cho xhote, Ufun.13:16-18. Msiba mkuu ni kwamba wengi wanaojiita Wakristo ndani ya Kanisa lililokengeuka watajisalimisha kwa madai ya masanamu ya kishetani yaw Mpinga Kristo, Ufun.14:9,10. Paulo analionya kanisa katika, 1Tim.4:1. Pia vile vile, Ezekieli anatabiri kwamba uzao wa asili wa Ibrahimu utachagua kuyaabudu masanamu haya, kabla ya ghadhabu ya Mungu haijawaangamiza, Ezek.7:19,20. Kristo pia anawaambia wanafunzi Wake kuhusu muda huu maalumu katika siku za mwisho, Math.24:9,10,12. 4.

Subira ya Watakatifu, Ufun.3:10

Katika wakati huo, subira na imani ya watakatifu itajaribiwa vilivyo tangia hapo katika historia ya kanisa, Ufun.13:10; 14:12. lakini Bwana anawapa watakatifu Wake waaminifu ahadi katika Ufun.3:10. Ndiyo maana, kanisa linaagizwa kwa umakini kabisa katika siku za mwisho, kudumu ndani Yake Yesu, ili Atakapoonekana tusiaibike, 2Yoh.2:28. Kwa wale watakatifu watakaovumilia katika kipimo cha Kishetani kwa wanadamu wote, kuna ushindi, Ufun.14:12,13. Watakatifu hawa hawataingia katika adhabu ya milele ambayo iko tayari kuijilia ulimwengu wa wasioamini katika Siku ya Bwana. Kwa hiyo, kabla ya ghadhabu ya Mungu haijamwagwa juu ya ulimwengu usioamini, Mungu atalinyakua kanisa Lake lenye subira, akiliondoa katika eneo la hatari. Ufun.3:10b,11a. Na baadaye ndipo ghadhabu Yake Mungu itamwagwa kwa wale watakaobakia duniani, wakati muhuri wa saba wa gombo mwisho utakapovunjwa.

Related Documents

Juma
November 2019 7
Juma
November 2019 2
Juma
June 2020 8
Danieli Leal
August 2019 18
La La La La La La La
July 2020 44