Namna Ya Kumaliza Tatizo La Kukoroma

  • Uploaded by: Vegemboga
  • 0
  • 0
  • May 2020
  • PDF

This document was uploaded by user and they confirmed that they have the permission to share it. If you are author or own the copyright of this book, please report to us by using this DMCA report form. Report DMCA


Overview

Download & View Namna Ya Kumaliza Tatizo La Kukoroma as PDF for free.

More details

  • Words: 276
  • Pages: 1
NAMNA YA KUMALIZA TATIZO LA KUKOROMA Habari za kazi mheshimiwa Michuzi, nilipitia hapa kwenye blog yako nikakuta bwana Chumaka wa Korogwe akiomba msaada wa namna ya kutatua tatizo lake la kukoroma ambalo linamnyima mkewe usingizi.Majibu mengine niliyoyasoma yalikua ya ajabu na pia hayakuweza kumsaidia bwana Chumaka. Na vifaa vingi vilivozungumzwa kwa mtu aliyopo Korogwe sidhani angevipata kwa urahisi. Kwakua kulikua na comments zaidi ya 35 nikahisi nikiweka na yangu pale wengi hawataiona,naomba uiweke peke yake ili iweze kusaidia watu kama mimi ilivyonisaidia. Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao. Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu. Mzee huyu aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake. Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.

Related Documents

Ya
November 2019 59
Ya
June 2020 29
Ya Ali Ya Hussain
July 2020 31
Hi Ya Ya
June 2020 23
Ya Rasoolallah Ya Ah
October 2019 34

More Documents from "waqar"