HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI TAARIFA MUHIMU TAARIFA
MAELEZO 90
45’na100
Mipaka
Wilaya ipo Latitude na 39o 50’ Mashariki
45’kusini mwa Ikweta na Longitudo 39o 45’
Eneo
Wilaya ina 945 KM2 sawa na asilimia 1.41%ya eneo lote la Mkoa wa Lindi lenye 67,000KM2
Eneo la Makazi, Kilimo na Mifugo
833 KM2 Sawa na asilimia 88% ya eneo lote la Wilaya ni nchi kavu; eneo linalofaa kwa Kilimo ni hekta 67,962 eneo lililobaki linafaa kwa kwa Makazi na Ufugaji na eneo la maji ni km2 112
Eneo la Hifadhi, Misitu na Wanyamapoli
Eneo la hifadhi ni 26.07KM2 sawa na asilimia 2.7% ya eneo lote la Wilaya.
Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ilikuwa na jumla ya Watu 78,841 Wanawake wakiwa ni 41,316 na Wanaume 37,525. Hivi sasa Manispaa inakadiriwa kuwa na Watu 134,100. Wanawake 70,268 na Wanaume 63,832. Wastani wa ukubwa wa Kaya ni watu 5 sawa na 0.02% ya kaya 26,820, Msongamano wa Watu katika eneo la Makazi (Population density) ni Watu 142 kwa KM2
Nguvu kazi
Wilaya ina Watu 64,368 (2016) wenye uwezo wa kufanya kazi (Nguvu kazi) yaani miaka 15-64, sawa na 48% ya idadi ya Watu wote kwa sasa.
Utawala
Manispaa ina Tarafa 3 Kata 20 Mitaa 117
Hali ya hewa
Hali ya hewa ya Wilaya ni ya Ki-tropiki, wastani wa joto ni 280c na wastani wa Mvua kwa mwaka ni kati ya 800mm hadi 1200mm
Uchumi wa Manispaa
80% ya wakazi wanategemea Kilimo,Uvuvi na Ufugaji. Pato la Wananchi ni la chini Ki-fedha. 55% ya wakazi wanaishi chini ya Dola 1 ya Ki-Marekani kwa siku.
Kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 na Marekebisho yake ya mwaka 2000, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi pamoja na mambo mengine ina wajibu wa Kukusanya Mapato kupitia Kodi, Leseni, Ada na Tozo mbalimbali zilizo ndani ya Mamlaka yake kisheria.